Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi wawakamata washukiwa wa mauaji ya mwanariadha raia wa Uganda

Nairobi – Polisi nchini Kenya mapema Jumatatu wamethibitisha kukamatwa kwa watu wawili wanaohusishwa na mauaji ya mwanariadha wa Uganda,  Benjamin Kiplagat, wikendi iliyopita.

Kiplagat mzawa wa Kenya alikuwa ameiwakilisha Uganda kimataifa katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi
Kiplagat mzawa wa Kenya alikuwa ameiwakilisha Uganda kimataifa katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi AFP - FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Wanaume hao wawili wanaoaminika kuwa na umri wa miaka 30 walikamatwa viungani mwa mji Eldoret katika mkoa wa bonde la ufa kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa eneo hilo Stephen Okal.

Kiplagat mzawa wa Kenya alikuwa ameiwakilisha Uganda kimataifa katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi, ikiwa ni pamoja na katika michezo kadhaa ya Olimpiki na mashindano ya dunia.

Mwili wa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 34 ulipatikana kwenye gari Jumamosi usiku ukiwa na jeraha kubwa la kisu shingoni.

Mmoja wa washukiwa alikuwa amekamatwa akiwa na kisu kinachoaminika kutumika katika mauaji hayo, idara ya polisi ilisema.

Kiplagat, ambaye taaluma yake ilidumu kwa takriban miaka 18, alishinda medali ya fedha katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji katika mashindano ya dunia ya vijana ya 2008 na shaba kwenye mashindano ya Afrika mnamo 2012.

Kifo chake kilifuatia mauaji ya Oktoba 2021 ya nyota wa mbio za masafa marefu Mkenya Agnes Tirop wakati huo akiwa na umri wa miaka 25 akiwa amedungwa kisu nyumbani kwake Iten, mjini Eldoret katika mkoa wa bonde la ufa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.