Pata taarifa kuu

Kenya: Washukiwa wawili wa mauaji ya Kiplagat watupwa jela

Wanaume wawili wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya mwanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat wiki iliyopita katika Bonde la Ufa nchini Kenya wamefikishwa mahakamani na kufungwa gerezani siku ya Jumanne.

Benjamin Kiplagat alifika nusu-fainali ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi kwenye Michezo ya Olimpiki ya London 2012.
Benjamin Kiplagat alifika nusu-fainali ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi kwenye Michezo ya Olimpiki ya London 2012. AFP - FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa hao wawili wenye umri wa miaka 25 na 30 walizuiliwa kwa siku 21 na mahakama katika mji wa Eldoret (Kenya), huku polisi wakiendelea na uchunguzi wao kuhusu mauaji ya mwanariadha huyo.

Polisi wa Kenya walitangaza siku ya Jumatatu kukamatwa kwa wanaume hawa wawili, wanaoelezewa kama "wahalifu wanaojulikana ambao waliwatishia watu", karibu na Eldoret ambapo mwili wa Kiplagat, aliyechomwa kisu shingoni, ulipatikana kwenye gari, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Ingawa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, polisi walisema mwathiriwa aliyekuwa akisafiri kwa gari "alishambuliwa" na watu hao wawili waliokuwa kwenye pikipiki.

Mji wa Eldoret katika Bonde la Ufa huwaona wanariadha wengi waliobobea katika mbio ndefu na za kati kuja kufanya mazoezi ili kunufaika na mwinuko. Kiplagat, mzaliwa wa Kenya na mwenye umri wa miaka 34, aliwakilisha Uganda katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi katika matoleo kadhaa ya Michezo ya Olimpiki na michuano ya dunia.

Katika miaka 18 ya maisha yake, Kiplagat alijitokeza katika kategoria za vijana, hasa kushinda medali ya fedha katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwenye mashindano ya vijana ya dunia mwaka wa 2008. Mshindi wa medali ya shaba katika michuano ya Afrika mwaka wa 2012, alifika nusu fainali kwenye Michezo ya Olimpiki ya London 2012 na pia alishiriki katika Michezo ya Rio miaka minne baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.