Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Mchungaji maarufu Uganda ajeruhiwa katika jaribio la mauaji

Mwinjilisti mashuhuri wa Uganda mchungaji Aloysius Bugingo, anayemuunga mkono Rais Yoweri Museveni, alijeruhiwa Jumanne jioni katika shambulio lililomuua mlinzi wake, polisi wa Uganda imetangaza leo Jumatano, ambayo imesema wanachunguza "jaribio la mauaji".

Mchungaji Bugingo pia ana vituo vyake vya televisheni na redio, anazotumia kuonyesha uungaji mkono wake usio na masharti kwa Rais Museveni na, hivi majuzi, kwa mwanawe Muhoozi Kainerugaba (kwenye picha), anayeonekana kuwa mrithi wa baba yake, mwenye umri wa miaka 79, kwenye kiti cha urais.
Mchungaji Bugingo pia ana vituo vyake vya televisheni na redio, anazotumia kuonyesha uungaji mkono wake usio na masharti kwa Rais Museveni na, hivi majuzi, kwa mwanawe Muhoozi Kainerugaba (kwenye picha), anayeonekana kuwa mrithi wa baba yake, mwenye umri wa miaka 79, kwenye kiti cha urais. © Hajarah Nalwadda / AP
Matangazo ya kibiashara

"Nimezungumza naye na yuko sawa. Alijeruhiwa kidogo kwenye bega la kushoto," Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais, amesema katika ujumbe kwenye X (zamani ikiitwaTwitter), akimshukuru Mungu kwamba "msaidizi huyu wa dhati" "alinusurika shambulio hilo baya".

Gari lake lilipigwa risasi mwendo wa saa tatu usiku (saa za Afrika Mashariki) siku ya Jumanne alipokuwa akiendesha gari katika mji mkuu Kampala, kulingana na polisi. "Washambuliaji wasiojulikana walilifyatulia risasi dhidi ya gari la Mchungaji Bugingo (....) kabla ya kukimbia haraka kwa pikipiki," amesema msemaji wa polisi katika mji mkuu, Luke Owoyesigire, katika taarifa.

"Ingawa alijeruhiwa katika shambulio hilo, Mchungaji Aloysius Bugingo alifanikiwa kulipeleka gari hilo katika hospitali ya Mulago. Kwa bahati mbaya, mlinzi wake, Muhumuza Richard, alifariki. (...) Kwa sasa, Mchungaji Bugingo anaendelea na matibabu na yuko chini ya uangalizi," polisi imeongeza. Walipofika kwenye eneo la tukio, wachunguzi "waligundua kuwa eneo la uhalifu lilikuwa limerekebishwa," taarifa kwa vyombo vya habari inabainisha.

Mchungaji Bugingo ni mtu mwenye utata nchini Uganda. Anaongoza House of Prayer Ministry, mojawapo ya makanisa ya Kipentekoste yenye ushawishi mkubwa katika nchi hiyo ya kidini ya Afrika Mashariki.

Pia ana vituo vyake vya televisheni na redio, anazotumia kuonyesha uungaji mkono wake usio na masharti kwa Rais Museveni na, hivi majuzi, kwa mwanawe Muhoozi Kainerugaba, anayeonekana kuwa mrithi wa baba yake, mwenye umri wa miaka 79, kwenye kiti cha urais.

Uungwaji mkono huu kwa rais, ambaye ameitawala Uganda kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1986, mara kwa mara huvutia hasira za upinzani, ambao huwakosoa waziwazi katika mahubiri yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.