Pata taarifa kuu

RDC: Mahakama kuamua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Ijumaa wiki hii

Nairobi – Mahakama ya kikatiba nchini DRC, inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi ya kupinga matekeo ya uchaguzi wa urais, tarehe 12 mwezi huu.

Afisi ya kiongozi wa mashataka nchini DRC, inataka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo ikisema haina msingi
Afisi ya kiongozi wa mashataka nchini DRC, inataka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo ikisema haina msingi AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Ni Kesi iliokuwa imewasilishwa mahakamani na mmoja wa wagombea Theodore Ngoy Ilunga, akitaka matekeo ya uchaguzi wa urais wa disemba 20, kufutwa kwa msingi kwamba ulikumbwa na matatizo mengi ya kiufundi na udanganyifu.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi huo tarehe 12 mwezi huu baada ya kuskiza kesi hiyo jumatatu, ambapo upande wa rais Felix Tshiesekedi aliyetengazwa mshindi wa uchaguzi huo kujitetea mahakama pamoja na tume ya uchaguzi CENI.

Félix Tshisekedi, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais
Félix Tshisekedi, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais AFP - ISSOUF SANOGO

Afisi ya kiongozi wa mashataka nchini DRC, inataka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo ikisema haina msingi .

Visa kadhaa vya udanganyifu wa kura viliripotiwa katika uchaguzi wa Urais nchini DRC, pamoja na ule wa wabunge na madiwani.

Licha ya kuonesha kutoridhishwa na matekeo ya uchaguzi wa urais,  wapinzani wakuu ambao ni Moïse Katumbi na Martin Fayulu haukufika mahakama kupinga matekeo hayo, wakidai mahakama ya kikatiba inaegemea upande wa serikali.

Moïse Katumbi, aliibuka watatu katika uchaguzi huo wa mwezi Desemba
Moïse Katumbi, aliibuka watatu katika uchaguzi huo wa mwezi Desemba AFP - ALEXIS HUGUET
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.