Pata taarifa kuu

Rais Museveni amezungumza kwa mara ya kwanza tangu nchi yake kuondolewa AGOA

Nairobi – Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema nchi yake itaendelea kufanya biashara na mataifa ya kigeni ambayo hayatakuwa yanaingilia uhuru wake, matamshi aliyoyatoa majuma kadhaa tangu Marekani iiondoe nchi yake katika mkataba wa kibiashara AGOA.

Yoweri Museveni- Rais wa Uganda
Yoweri Museveni- Rais wa Uganda AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Tangu atie saini sharia tata kuhusu ushoga, rais Museveni amekuwa katika shinikizo kutoka kwa mataifa ya magharibi yanayotaka abatilishe sharia hiyo, ambayo wanasema inakiuka haki za binadamu.

Marekani ilitishia kwa mara ya kwanza kuiwekea vikwazo Uganda na kuiondoa  kutoka kwa mkataba wa biashara wa AGOA mwezi Mei, baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupitisha sheria yenye utata dhidi ya ushoga.

Sheria inatoa adhabu ya kifo kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Uganda
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Uganda AP

"Kwa sasa, wale wanaotuwekea shinikizo, wanapoteza muda wao. Hatupaswi kuwa na wasiwasi kuhusu hilo," Rais Museveni alisema katika hotuba yake ya kitaifa siku ya Jumanne, akizungumza kwa mara ya kwanza tangu nchi yake kuondolewa kwenye mpango huo.

Katika hatua nyingine rais Museveni, katika hotuba yake ya mwaka mpya, amezungumzia vita ya nchi yake dhidi ya waasi wa ADF nchini DRC.

‘‘ADF hawana nafasi ya kufaulu, tumewaangamiza wote kwa awau ya kwanza, ya pili  na ya tatu na sasa tuko kwa awamu ya nne.’’ alisema rais Museveni.

00:37

YOWERI MUSEVENI SNIP 10 01 2024 KUHUSU ADF

Kundi la waasi wa ADF limekuwa likitekeleza mashambulio katika eneo la mpaka wa nchi ya Uganda na DRC haswa katika eneo la Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.