Pata taarifa kuu

RDC: Wabunge wa Ensemble pour le République kuhudhuria vikao vya bunge

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chama cha upinzani cha Ensemble pour le République kinachoongozwa na Moise Katumbi aliyemaliza wa pili kwenye uchaguzi wa urais mwaka uliopita, kimeamua kuwa na wawakilishi wake kwenye bunge la kitaifa, majimbo na manispaa, watahudhuria vikao kwenye mabunge hayo.

Chama hiki cha upinzani kina wawakilishi 23 peke Kati ya 500 kwenye bunge la kitaifa
Chama hiki cha upinzani kina wawakilishi 23 peke Kati ya 500 kwenye bunge la kitaifa AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

 

Hatua hii inakuja baada ya mashauriano ya siku mbili jijini Lubumbashi.

Wanasiasa zaidi ya 50 wakiwemo walioteuliwa kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Ensemble pour la République walichukua siku mbili ya mazungumzo yalioongozwa na Moise Katumbi.

Gratien Iracan, ni mbunge aliyechanguliwa katika mji wa Bunia.

“Tunapenda kuheshimu raia waliotuchagua na katiba na inatubidi kuangalia ili tusifikie hatua hii maana ni jambo ambalo litarudisha nyuma nchi yetu na linaweza kuleta vita.” alisema Gratien Iracan.

00:24

Gratien Iracan, mbunge aliyechanguliwa katika mji wa Bunia

Katika bunge la Kitaifa, chama hiki cha upinzani kina wawakilishi 23 peke Kati ya 500. Licha ya hayo, Clotilde Mutita mbunge wa huko Lubumbashi anasema sauti ya upinzani itasikika bungeni.

“Japokuwa tupo wachache, hatuwezi kukata tamaa, Congo ni nchi yetu sisi wote, naomba kuwa na matumani.” alieleza Clotilde Mutita.

00:14

Clotilde Mutita mbunge wa huko Lubumbashi

Chama cha Moise Katumbi pia kinaendelea kushtumu namna uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba kikitoa wito kwa wanaodaiwa kuhitilafiana na uchaguzi huo kakamatwa na kuwajibishwa.

Denise Maheho-RFI Kiswahili, Lubumbashi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.