Pata taarifa kuu

Rwanda yalalamikia kutoshirikishwa kwa mazungumzo ya kuidhinishwa kikosi cha SAMIDRC

Nairobi – Wizara ya Mambo ya nje nchini Rwanda, imeiandikia barua Tume ya Umoja wa Afrika, kulalamikia kutoshirikishwa kwenye mazungumzo ya kuidhinishwa kikosi cha jeshi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika SAMIDRC, kutumwa Mashariki mwa DRC ili kupambana na makundi ya waasi.

Rwanda imeandika barua hii, wakati hii serikali ya Kinshasa  na mataifa ya Magharibi, yakiishtumu kwa kuwaunga mkono waasi wa M 23
Rwanda imeandika barua hii, wakati hii serikali ya Kinshasa  na mataifa ya Magharibi, yakiishtumu kwa kuwaunga mkono waasi wa M 23 REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta kupitia barua, aliyomwandikia Mwenyekiti wa Tume ya Umoja ya Umoja wa Afrika Moussa Faki imeonesha masikitiko ya nchi yake kutohusishwa kwenye mazungumzo ya kujadili ujio wa kikosi cha SADC Mashariki wma DRC.

Biruta amesema kwa sababu Rwanda haikualikwa, ilikuwa ni muhimu kwa Tume hiyo kufahamu kuwa, kikosi hicho cha SADC kinachopigana kwa msaada wa jeshi la DRC, kinaungwa mkono na kundi la FDLR lililotekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Aidha, amesisitiza kuwa kundi hilo linasalia hatari kwa usalama wa Rwanda, na limeendeleza harakati za kujaribu kuinagusha serikali ya Kigali, likiwa kwenya ardhi ya DRC.

Ili kupata suluhu ya utovu wa usalama Mashariki mwa DRC, Rwanda inataka kiini cha mzozo huo kwa serikali ya Kinshasa kukubali mikataba ya kuleta amani kwa njia ya kisiasa na mazungumzo iliyotiwa saini jijini Nairobi na Luanda kuheshimiwa, huku ikiilaumu Jumuiya ya Kimataifa kwa kupuuza chanzo cha utovu huo wa usalama kwa makusudi.

Rwanda imeandika barua hii, wakati hii serikali ya Kinshasa  na mataifa ya Magharibi, yakiishtumu kwa kuwaunga mkono waasi wa M 23 kwa kuwapa silaha na kutuma  vikosi vyake Mashariki mwa DRC, madai ambayo Kigali imeendelea kukanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.