Pata taarifa kuu

Kenya: Serikali kuwasaidia raia walioathiriwa na mafuriko kuendelea na maisha

Rais wa Kenya, William Ruto, amewahakikisha raia waliothiriwa na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo, kuwa hawatalala njaa na kwamba Serikali yake itawasaidia kujikimu hadi pale watakaporejea katika hali ya kawaida.

Mamia ya raia wa Kenya wamepoteza makazi yao baada ya kuja maji yanayotokana na mvua kubwa.
Mamia ya raia wa Kenya wamepoteza makazi yao baada ya kuja maji yanayotokana na mvua kubwa. © REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Akitembelea maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko, rais Ruto, amewataka raia kuondoka kwa hiari katika maeneo hatarishi.

Kauli yake, ameitoa wakati huu mamlaka za hali ya hewa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, zikionya kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa mvua zaidi, ambapo hadi sasa watu zaidi ya 400 wameripotiwa kufariki kwenye ukanda huo na wengine maelfu hawana makazi.

“Hakuna mwanachi kabisa mwanachi atalala njaa na tutaleta chakula ya kutosha kila mwanachi apate chakula na tayari tumeweka pesa ya kutosha ya kununua chakula.” alisema Rais William Ruto.

00:42

Rais William Ruto kuhusu waathiriwa wa mafuriko

Haya yanajiri wakati huu idadi ya watu waliofairki kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa ikifikia zaidi ya 220.

Licha ya Kenya na Tanzania kuepuka athari za kimbunga Hidaya ambacho nguvu zake zilipungua, serikali ya Nairobi imeonya dhidi ya kuendelea kushuhudiwa kwa mvua kubwa ikiwataka raia wake kuchukua tahadhari.

Soma piaIdadi ya waliofariki katika mafuriko nchini Kenya imefikia 228

Magharibi ya Kenya, mto Nyando ulivunja kingo zake Jumapili ya wikendi iliopita na kusababisha mafuriko katika kituo cha polisi, hospitali, shule na soko la Ahero katika kaunti ya Kisumu kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Tayari serikali ya Kenya imewataka watu wanaoishi karibu na mito, mabwawa au sehemu zilizo kwenye hatari za kukabiliwa na mafuriko na mapromoko ya udongo kuondoka.

Serikali pia imeonya uwezekano wa kutokea kwa magonjwa yanayotokana na maji chafu, kisa kimoja na kipindupindu kikiripotiwa sawa na ugonjwa wa kuharisha.

Mamlaka nchini humo imetuhumiwa kwa kutoweka tayari mikakati ya kupambana na athari za mafuriko licha ya kuwepo kwa onyo la kutokea kwa mvua kubwa kutoka wa idara ya hali ya hewa.

Mafuriko yameathiri kwa sehemu kubwa usafiri jijini Nairobi.
Mafuriko yameathiri kwa sehemu kubwa usafiri jijini Nairobi. © Monicah Mwangi / REUTERS

Tayari muungano wa upinzani Azimio la Umoja umeitaka serikali ya rais Ruto kutangaza suala la mafuriko kuwa janaga la kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.