Pata taarifa kuu

Kenya: Serikali na madaktari wanaogoma wametakiwa kuafikia suluhu mara moja

Mahakama ya kazi nchini Kenya, hapo jana ilitoa saa 48 kwa Serikali na madaktari walioko katika mgomo kufikia makubaliano ya namna watakavyorejea kazini na kumaliza mgomo wa waguzi wa afya unaofanyika nchi nzima.

Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara.
Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara. REUTERS - Monicah Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Katika maelekezo yake, jaji anayesikiliza shauri hilo, amesema ikiwa muda huo utamalizika bila muafaka, basi itasikiliza mashauri ya pande zote mbili na kutoa uamuzi.

Kwa upande wao Madaktari licha ya kuonesha utayari wa kurejea kwenye meza ya mazungumzo, katibu mkuu wa muungano wa KMPDU, Davji Attelah, anasema hawatalegeza Kamba ikiwa Serikali haitatekeleza mkataba wa mwaka 2017.

“Jukumu letu ni kuendelea na mgomo hadi pale ambapo tutapata suluhu ya kurejea kazini na kama tulivyosema, makubaliano yetu yamejikita katika mkataba wa CBA.” alisema Davji Attelah.

00:43

katibu mkuu wa muungano wa KMPDU, Davji Attelah

Mazungumzo kati ya madktari hao wanaogoma na serikali yamekosa kupata suluhu, wagonjwa wakiendelea kuangaika katika hospitali za umma kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Karibia wanachama elfu saba wa chama cha madaktari nchini humo (KMPDU) walianza mgomo wa kitaifa katikati ya mwezi Machi wakitaka kuboreshwa kwa mazingira yao kazi ya kuongezewa mshaara.

Aidha wanataka kutekelezwa kikamilifu kwa makubaliano yam waka wa 2017 yalioafikiwa baada ya mgomo mwengine uliofanyika mwaka huo.

Soma piaMazungumzo kati ya serikali na madaktari kumaliza mgomo wa kitaifa yamekwama

Mgomo wa wadumu wa afya kuhusu kuboreshwa kwa mazingira ya kazi katika hospitali za umma umekuwa ukishuhudiwa nchini kenya, baadhi yao wakilazimika kuhamia katika nchi zengine kutafuta malipo bora.

Mwaka wa 2017, madaktari walishiriki mgomo mwengine wa siku 100 kote nchini hali iliopelekea hospitali zote za umma kufungwa.

Wagonjwa waliokuwa wamelazwa wakati huo waliripotiwa kufariki wakati wa mgomo huo ambao baadaye ulimalizika baada ya makubaliano kati ya pande mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.