Pata taarifa kuu
TANZANIA-KATIBA

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuhutubia bunge la katiba hii leo mjini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma leo Ijumaa, baada ya rasimu ya pili ya katiba mpya kuwasilishwa bungeni mapema juma hili. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya rais Kikwete imekuwa ikisubiriwa na wajumbe wa bunge la Katiba nchini humo pamoja na wananchi wa Tanzania, wanaotaka kusikia mtazamo wa rais wao kuhusu maswala mbalimbali hasa suala nyeti la muunndo wa serikali.

Karibu mwezi mmoja sasa wajumbe hao wamekuwa wakijadiliana na kukubaliana kuhusu kanuni zitakazowaongeza wakati wakapioanza kujadil rasimu ya Katiba mpya.

Siku ya Alhamisi, wajumbe hao walipata uzoefu wa namna ya wakneya walivyopata Katiba mpya.

Akizungumza na wabunmge hao mjini Dodoma aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya Amos Wako aliwaambia kuwa wahakikishe kuwa rasimu itakayopitishwa na bunge hilo izingatie maoni ya wananchi.

Tanzania itakuwa nchi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya katika siku za hivi karibuni, kujihusiha na mchkato wa upatikanaji wa Katiba mpya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.