Pata taarifa kuu
UN-YEMEN-MSAADA-JAMII

Yemen : UN yaanza kutoa misaada ya kibinadamu leo Ijumaa

Umoja wa Mataifa umetangaza siku sita za kutoa misaada ya kibinadamu nchini Yemen kuanzia leo Ijumaa.

Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.
Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi
Matangazo ya kibiashara

Misaada hiyo inatarajiwa kutolewa katika maeneo yaliyaothiriwa na machafuko yanayoendelea hadi mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani juma lijalo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa misaada hiyo inastahili kuwafikia wahanaga haraka iwezekanavyo baada ya waasi na wanajeshi wa serikali kukubaliana kusitisha makabiliano kwa muda.

Zaidi ya watu elfu tatu wamepoteza maisha katika makabiliano hayo toka mwezi Machi mwaka huu.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Yemen iliyokimbilia ukimbizni, hivi karibuni iliambia Umoja wa Mataifa kuwa iko tayari kusitisha vita kwa muda ili kumaliza machafuko ya miezi mitatu yanayoendelea.

Msemaji wa serikali hiyo ya Yemen Rajeh Badi alimwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuwa, serikali hiyo ingependa mwafaka huo kuanza kutekelezwa kwa siku chache zijazo kwa sababu za kibinadamu.

Serikali ya Yemen, ilisema iko tayari kuwaachilia huru waasi wa Kihouthi wanaoshikiliwa ambao wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali.

Kiongozi wa kundi la waasi Zeifullah al-Shami amesema kuwa masharti ya serikali hayo hayakubaliki.

Wito huu wa serikali ya Yemen unakuja wakati huu kukiwa na mpango wa kuendelea kwa mazungumzo ya amani siku ya Jumapili mwishoni mwa juma hili kati ya serikali na waasi jijini Geneva.

Machafuko nchini Yemen yamekuwa yakiendelea kwa miezi mitatu na zaidi ya watu elfu tatu wamepoteza maisha kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.