Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-GENEVA-MAZUNGUMZO-SIASA

Yemen: IS yakiri kutekeleza mashambulizi matano Sanaa

Wakati ambapo mazungumzo ya amani yameendelea kushindikana mjini Geneva kati ya pande zinazohusika katika mgogoro nchini Yemen, mji mkuu wa Sanaa umeendelea kukabiliwa na mdororo wa usalama.

Mtu anayebebelea silaha akitazama moja ya magari yaliyolipuka katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, Jumatano Juni 17.
Mtu anayebebelea silaha akitazama moja ya magari yaliyolipuka katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, Jumatano Juni 17. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Sanaa ilikumbwa na mashambulizi matano. Mashambulizi hayo yamelenga pia misikiti na nyumba ya kiongozi wa waasi wa Huthi. Mashambulizi haya yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State yanasadikiwa kuwaua zaidi ya watu thelathini.

Mashambulizi haya yameendeshwa kwa wakati mmoja. Magari mawili yaliyotegwa mabomu yamelipuka nje ya misikiti miwili, na vilipuzi vingine viliwekwa katika milango ya misikiti mingine miwawili wakati ambapo waumini walikua wakijianda kuhudhuria sala ya jioni.

Moja ya misikiti ulilengwa mwezi Machi na mashambulizi yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State, mashambulizi ambayo yaliwaua zaidi ya watu 140. Mashambulizi yaote haya yaliyoendeshwa kwa wakati mmoja yanadaiwa kutekelezwa na kundi moja ambalo ni Islamic State.

Kwa mujibu wa mshahidi na Idara za usalama, gari nyingine ndogo lililokua lilitegwa bomu ililipuka nje ya nyumba ya mkuu wa ofisi ya tawi la kisiasa la waasi wa Huthi katika mji wa Sanaa. Picha za misikiti iliyoteketezwa kwa moto zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, na inasadikiwa kuwa mashambulizi hayo yaliwaua zaidi ya watu thelathini.

Mashambulizi haya yanatokea katika usiku wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhan wakati ambapo mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa mjini Geneva na Umoja wa Mataifa kati ya pande zinazohusika katika mgogoro yameendelea kushindikana. Mashambulizi hayo pia yanatokea siku moja Baada ya kutangazwa kifo, wiki iliyopita, cha kiongozi wa al Qaeda katika Peninsula ya Arabia, Nasser al-Wahishi, aliyeuawa na ndege ya Marekani isiyo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.