Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HUTHI-VITA-SIASA

Yemen: mazungumzo ya amani yaahirishwa

Mazungumzo ya amani kuhusu hali ya kisiasa na usalama nchini Yemen yaliyoratibiwa kufanyika juma lijalo jijini Geneva yameahirishwa.

Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.
Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi
Matangazo ya kibiashara

Mazunguzo hayo yameahirishwa kutokaana na mapigano yanayoendelea kati ya wanajeshi wanaoongozwa na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alitarajiwa kufungua mazungumzo hayo lakini sasa haifahamiki ni lini yatafanyika.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema Umoja wa mataifa ungeoamba mazungumzo hayo kuanza baada ya mapigano kusitishwa.

Mapigano yalianza tena Jumatatu wiki hii baada ya siku tano za kutoa misaada kwa waathiriwa wa mapigano kukamilika.

 

Mashambulizi haya mapya yanakuja baada ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa wa mapigano hayo.

Saudi Arabia imeanza mashambulizi hayo mjini Aden Kusini mwa nchi hiyo wakati huu wanasiasa nchini humo wakianza kujadiliana kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa suluhu ya kisiasa nchini humo.

Mkataba wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano ili kuruhusu misaada ya kiutu kuwafikia walengwa nchini Yemen ulianza kutekelezwa tangu Juamnne usiku wiki hii.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kuanzisha tena mazungumzo kwa ajili ya ufumbuzi wa kisiasa nchini Yemen, aliwasili Jumanne wiki iliyopita katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Ismaïl Ouled Cheikh Ahmed, aliwasili Jumanne wiki iliyopita katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, ili kujaribu kuanzisha mazungumzo kati ya viongozi wa Yemen na waasi wa Kishia wa Huthi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.