Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Mapigano yashuhudiwa Yemen

Wanajeshi wa Sudi Arabia wakishrikiana na washirika wake wamenza tena mashambulizi ya angaa dhidi ya waasi wa Kihuthi nchini Yemen.

Ndege ya jeshi la Saudi Arabia ikishiriki katika mashambulizi dhidi ya waasi wa Huthi, Yemen, Aprili 2 mwaka 2015.
Ndege ya jeshi la Saudi Arabia ikishiriki katika mashambulizi dhidi ya waasi wa Huthi, Yemen, Aprili 2 mwaka 2015. REUTERS/Saudi Press Agency
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya mapya yanakuja baada ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa wa mapigano hayo.

Saudi Arabia imeanza mashambulizi hayo mjini Aden Kusini mwa nchi hiyo wakati huu wanasiasa nchini humo wakianza kujadiliana kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa suluhu ya kisiasa nchini humo.

Mkataba wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano ili kuruhusu misaada ya kiutu kuwafikia walengwa nchini Yemen ulianza kutekelezwa tangu Juamnne usiku wiki hii.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kuanzisha tena mazungumzo kwa ajili ya ufumbuzi wa kisiasa nchini Yemen, aliwasili Jumanne wiki iliyopita katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Ismaïl Ouled Cheikh Ahmed, aliwasili Jumanne wiki iliyopita katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, ili kujaribu kuanzisha mazungumzo kati ya viongozi wa Yemen na waasi wa Kishia wa Huthi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.