Pata taarifa kuu
YEMEN--HOUTHI-MAZUNGUMZO-SIASA

Yemen : Ban Ki-moon atoa wito wa kusitisha mapigano

Mazungumzo kuhusu Yemen jijini Geneva yameingiliwa na kizungumkuti kutokana na kuchelewa kwa ujumbe wa waasi wa Kishia wa Huthi. Lakini bila hata hivyo kusubiri kuwasili kwa waasi hao, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Yemen.

Ban-Ki-moon " nina imani kwamba wiki hii itakua mwanzo wa mwisho wa mapigano".
Ban-Ki-moon " nina imani kwamba wiki hii itakua mwanzo wa mwisho wa mapigano". REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki-moon ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigani kwa kipindi cha wiki mbili ili kuruhusu misaada ya kibinadam kuwafikia walengwa hasa katika mwezi Ramadhan, ambao ni mwezi Mtukufu kwa Waislamu na unatazamiwa kuanza wiki hii.

“ Nina imani kuwa wiki hii itakua mwanzo wa mwisho wa mapigano ”, amesema Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, kabla ya kikao hiki cha mwanzo cha mazungumzo kati ya pande mbili zinazohusika katika mgogoro unaoendelea nchini Yemen: upande mmoja rais aliye uhamishoni, Abd Rabbo Mansour Hadi, ambaye anaungwa mkono na Saudi Arabia inayoongoza muungano wa nchi za kiarabu zinazoendesha vita nchini yemen tangu mwezi Mach uliyopita na upande mwenine waasi wa Huthi na washirika wake ambao waliuvamia mji mkuu wa Yemen, Sanaa mwezi Septemba mwaka 2014.

Ujumbe wa waasi haujawasili jijini Geneva kushiriki mazungumzo hayo kutokana na "Matatizo ya vifaa," chanzo cha Umoja wa Mataifa kimesema. Mazungumzo yalikua yanatazamiwa kuanza baadaye leo Jumatatu alaasiri.

Itakuwa kwa sasa suala la rasimu ya kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia walengwa. Kiasi kwamba majadiliano ya kwanza kati ya kambi mbili yatafanyika kupitia mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, kutoka Mauritania Ismail Ould Cheikh Ahmed, ambaye alipanga kukutana kwa mazungumzo na ujumbe ambao hautazungumza moja kwa moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.