Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA

Yemen yaendelea kukumbwa na mashambulizi ya angani

Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zimewashambulia waasi wa Yemen mapema Jumatatu alfajiri wikihii, ikiwa ni pigo jipya kwa mpango uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa wa kusitisha mapigano katika nchi hiyo ambayo mamilioni ya watu wanakabiliwa na kitisho cha baa la njaa.

Jengo la Wizara ya Ulinzi ya Sanaa liliharibiwa katika mashambulizi ya mabomu ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, Yemen Juni 10 mwaka 2015.
Jengo la Wizara ya Ulinzi ya Sanaa liliharibiwa katika mashambulizi ya mabomu ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, Yemen Juni 10 mwaka 2015. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya muungano huo yaliilenga ngome ya waasi wa Houthi, ya Saada, kaskazini mwa Yemen, pamoja na maeneo mengine ya waasi kusini mwa mji mkuu Sanaa na mkoa wa kusini wa Lahj.

Haijajulikana hasara iliyosababishwa na mashambulizi hayo. Mpango wa kusitisha vita kati ya pande hiz mbili uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa ulianza kutekelezwa Ijumaa usiku na unatarajiwa kudumu hadi Julai 17. Lakini wadadisi wanasema mpango huo unaohitajika kwa ajili ya kuwafikishia msaada wa dharura watu wanaotishiwa na baa la njaa, umekiukwa kutokana na mashambulizi yanayofanywa na muungano wa Saudia na mapigano ya ardhini.

Juma lililopita msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema kuwa misaada hiyo inastahili kuwafikia wahanga haraka iwezekanavyo baada ya waasi na wanajeshi wa serikali kukubaliana kusitisha makabiliano kwa muda.

Zaidi ya watu elfu tatu wamepoteza maisha katika makabiliano hayo toka mwezi Machi mwaka huu.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Yemen iliyokimbilia ukimbizni, hivi karibuni iliambia Umoja wa Mataifa kuwa iko tayari kusitisha vita kwa muda ili kumaliza machafuko ya miezi mitatu yanayoendelea.

Msemaji wa serikali hiyo ya Yemen Rajeh Badi alimwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuwa, serikali hiyo ingependa mwafaka huo kuanza kutekelezwa kwa siku chache zijazo kwa sababu za kibinadamu.

Serikali ya Yemen, ilisema iko tayari kuwaachilia huru waasi wa Kihouthi wanaoshikiliwa ambao wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali.

Kiongozi wa kundi la waasi Zeifullah al-Shami alisema kuwa masharti hayo ya serikali hayakubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.