Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-VITA-USALAMA

Kushiriki kijeshi kwa Urusi Syria kwaibua masuala mengi

Urusi ilikubali hivi karibuni kuipa Syria nyenzo za vita na uwepo wa wanajeshi wake nchini humo, lakini imekanusha kwamba askari wake wamekua wakishiriki katika vita vya nchi kavu na angani nchini Syria.

REUTERS/Alexei Nikolsky/RIA Novosti/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vingi, hata hivyo, vinathibitisha ushiriki mkubwa wa Urusi katika vita kwa upande wa serikali ya Syria.

Taarifa juu ya kuongezeka kwa uwepo wa wanajeshi wa Urusi nchini Syria pia imetolewa na maafisa wa Marekani na Ulaya maafisa, hata kwa vyanzo vilio karibu na serikali ya Syria, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Beirut, Paul Khalifeh. Urusi, imekanusha kuhusika kwake katika vita nchini Syria, lakini imekubali kuipa vifaa vya kijeshi.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, nyezo mbalimbali za kijeshi pamoja na magari ya kivita, vimepewa Syria chini ya mikataba iliyoafikiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini kati ya nchi hizo mbili. Vyanzo vya karibu na serikali ya Syria vinaonyesha kuwa jeshi la Syria limepokea hivi karibuni magari kadhaa ya kivita aina ya BTR 82 A na malori aina ya Ural. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Urusi pia amethibitisha kuwepo kwa washauri na wakufunzi wa kijeshi nchini Syria.

Lakini mabli na misaada hiyo ya nyenzo za kijeshi, kuna taarifa ya upanuzi wa uwanja mdogo wa ndege wa kijeshi wa Latakia, kwenye mwambao wa Mediterranean, ambao umekua ukifanyiwa ukarabati na kampuni ya ujenzi ya Urusi. Uvumi mwengine unathibitisha kwamba wataalamu wa Urusi wametembelea mji wa pwani wa Jable, kujifunza uwezekano wa kujenga kambi mpya ya jeshi la majini, pamoja na ile ya Tartus, inayoumiwa na jeshi la majini la Urusi tangu mwaka 1971.

Kama taarifa hizi zikithibitishwa, ina maana kwamba Urusi inajianda kwa vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuimarisha uwepo wake wa kijeshi nchini Syria, katika hali ya kujiweka sawa na kuwa na idadi kubwa, kwa kisingizio cha kupambana dhidi ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.