Pata taarifa kuu
HAKI-AMANI

Israel kujitetea dhidi ya tuhuma za mauaji ya kimbari Gaza

Israel itajibu Ijumaa hii, Januari 12, kwa kile nchi hiyo inachoeleza kuwa ni madai ya "kinyama" kwamba inafanya "mauaji ya halaiki" huko Gaza, katika kesi ya kihistoria ya kisheria iliyowasilishwa na Afrika Kusini mbele ya mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa.

Rafah, Januari 10, 2024.
Rafah, Januari 10, 2024. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

AfΕ•ika Kusini iliwasiliana na chombo hiki cha mahakama cha Umoja wa Mataifa mwezi uliopita kukiomba kutoa uamuzi juu ya uwezekano wa vitendo vya "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza.

Siku ya Alhamisi Afrika Kusini iliomba Mahakama ya Dunia kuamuru Israel isitishe mara moja operesheni yake ya kijeshi huko Gaza, ambapo inadai kuwa Israel ina "nia ya mauaji ya kimbari" dhidi ya raia wa Palestina. Israel inatarajia kujibu madai hayo leo ya Ijumaa.

onald Lamola, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, alikuja na wanasheria kadhaa. Kwa muda wa saa tatu, walitaka kuthibitisha kwamba mauaji ya halaiki yanaendelea huko Gaza.

Hamas si taifa na kwa hivyo haiwezi kuanzisha kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), hivyo ni wajibu wetu kuleta hali ya Gaza mbele yenu, wawakilishi wa Afrika Kusini wameeleza.

Mmoja baada ya mwingine, mawakili na wanasheria - wa Afrika Kusini au la - wameelezea mateso waliyovumilia Wapalestina huko Gaza tangu mashambulizi ya Israeli.

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, ukatili wowote unaoweza kufanywa, hakuna shambulio lolote linaloweza kuhalalisha matukio na vitendo vinavyotokea Gaza.

"Israel ina nia ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza," alisema Tembeka Ngcukaitobi, wakili katika Mahakama Kuu ya Afrika Kusini siku ya Alhamii.Β 

Afrika Kusini imejikita katika imani kwamba adui si Hamas pekee, bali amejikita katika mfumo wa maisha ya Wapalestina huko Gaza.

Mawakili wa Afrika Kusini walisema Israel kwa hiyo inafanya mauaji ya halaiki kwa kusudi huko Gaza na inakusudia kuendelea ikiwa tutaamini matamshi yaliyotolewa, maoni kutoka kwa mawaziri wa Israeli au maafisa wa jeshi.

Gambia ilifanya kama Afrika Kusini mwaka wa 2019: utaratibu dhidi ya Burma kuhusiana na Warohingya. Afrika Kusini inatumai kuwa majaji watafanya kama walivyofanya kwa Warohingya, ambapo ni kusema kuweka hatua za dharura.

Afrika Kusini inasema hatua hizi zinahitajika mara moja. Kwa sababu Mahakama itachukua muda mrefu kuamua iwapo kuna mauaji ya halaiki au la huko Gaza. Kikao cha pili kitafanyika siku ya Ijumaa hii na itakuwa zamu ya Israel kuwasilisha utetezi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.