Pata taarifa kuu

Shutuma za 'mauaji ya halaiki' dhidi ya Israeli: Afrika Kusini yatetea hoja zake mbele ya ICJ

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imejadili hali ya Gaza, baada ya Afrika Kusini kuamua kuzindua utaratibu huu chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mauaji ya Kimbari. Maafisa wa Afrika Kusini wanabaini kwamba Israel inafanya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza. Siku hii ya kwanza ya kusikilizwa Afrika Kusini imejitolea kuwasilisha hoja zao kuomba hatua za dharura.

Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, na ujumbe wake, mjini The Hague (Uholanzi) Januari 11, 2024, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, na ujumbe wake, mjini The Hague (Uholanzi) Januari 11, 2024, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki. REUTERS - THILO SCHMUELGEN
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet

Ronald Lamola, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, alikuja na wanasheria kadhaa. Kwa muda wa saa tatu, walitaka kuthibitisha kwamba mauaji ya halaiki yanaendelea huko Gaza.

Hamas si taifa na kwa hivyo haiwezi kuanzisha kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), hivyo ni wajibu wetu kuleta hali ya Gaza mbele yenu, wawakilishi wa Afrika Kusini wameeleza.

Mmoja baada ya mwingine, mawakili na wanasheria - wa Afrika Kusini au la - wameelezea mateso waliyovumilia Wapalestina huko Gaza tangu mashambulizi ya Israeli.

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, ukatili wowote unaoweza kufanywa, hakuna shambulio lolote linaloweza kuhalalisha matukio na vitendo vinavyotokea Gaza.

"Israel ina nia ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza," amesema Tembeka Ngcukaitobi, wakili katika Mahakama Kuu ya Afrika Kusini. Afrika Kusini "inaonekana wazi katika jinsi shambulio hili la kijeshi linavyotekelezwa," amesema.

Imejikita katika imani kwamba adui si Hamas pekee, bali amejikita katika mfumo wa maisha ya Wapalestina huko Gaza.

Mawakili wa Afrika Kusini wanasema Israel kwa hiyo inafanya mauaji ya halaiki kwa hiari huko Gaza na inakusudia kuendelea ikiwa tutaamini matamshi yaliyotolewa, maoni kutoka kwa mawaziri wa Israeli au maafisa wa jeshi.

Lakini ICJ haitatoa uamuzi hivi karibuni juu ya ukweli wa mauaji ya kimbari huko Gaza. Kwa upande mwingine, Afrika Kusini inaomba majaji waamuru hatua tisa za dharura ambazo zingetumika katika wiki moja baada ya kutangazwa kwao.

Miongoni mwa hatua nyingine za dharura, Mahakama lazima, kulingana na Afrika Kusini, iamuru kusitishwa kwa operesheni za Israel, kuhakikisha kwamba Wapalestina wanaweza kupata maji, chakula, umeme, huduma za afya, au kuhifadhi ushahidi wa mauaji ya kimbari.

Gambia ilifanya kama Afrika Kusini mwaka wa 2019: utaratibu dhidi ya Burma kuhusiana na Warohingya. Afrika Kusini inatumai kuwa majaji watafanya kama walivyofanya kwa Warohingya, ambapo ni kusema kuweka hatua za dharura.

Afrika Kusini inasema hatua hizi zinahitajika mara moja. Kwa sababu Mahakama itachukua muda mrefu kuamua iwapo kuna mauaji ya halaiki au la huko Gaza. Kikao cha pili kitafanyika siku ya Ijumaa hii na itakuwa zamu ya Israel kuwasilisha utetezi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.