Pata taarifa kuu
PAPA WEMBA

Nguli wa muziki wa Rhumba, Papa Wemba afariki dunia

Nguli wa muziki wa Rhumba raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kama Papa Wemba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini Cote d' Ivoire alikokuwa akishiriki tamasha la Femua. 

Mfalme wa Rhumba, Marehemu Papa Wemba enzi ya uhai wake akihojiwa na idhaa ya RFI
Mfalme wa Rhumba, Marehemu Papa Wemba enzi ya uhai wake akihojiwa na idhaa ya RFI RFI
Matangazo ya kibiashara

Papa Wemba alifariki dunia saa chache baada ya kuanguka akiwa jukwaani akitumbuiza mashabiki waliofurika kumshuhudia yeye pamoja na bendi yake, ambapo wacheza shoo wake walikuwa wakiendelea kucheza wasijue ni kipi kimemsibu kiongozi wao.

Akizungumza na Idhaa pamoja na kituo chetu mama cha France24, meneja wa mwanamuziki huyo amethibitisha Papa Wemba kufariki dunia jana usiku wakati alipokimbizwa hospitalini baada ya kuanguka jukwaani mjini Abidjan.

Papa wemba ambaye jina lake la kuzaliwa ni Jules Shungu Wembadio Pene Kibumba, ametangazwa kufariki siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 66.

Nguli huyu wa muziki amekuwa kwenye sanaa ya muziki barani Afrika toka mwaka 1969, ambapo amejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na staili yake ya muziki wa rhumba.

Ni mwanzilishi wa vuguvugu kubwa la muziki nchini DRC linalofahamika kama Viva la Musica pamoja na vuguvugu la Sapeur ambapo wanachama wake wengi ni vijana wanaotumia fedha nyingi kwaajili ya kununua mavazi.

Mwaka 2004 alihukumiwa na mahakama nchini Ufaransa kwa ushiriki wake wa kuwaingia raia wa DRC kinyume cha sheria nchini Ufaransa na kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela.

Miongoni mwa vibao vilivyompa umaarufu mkubwa duniani ni pamoja na kile cha "Rail On", A La Une na vibao vingine vingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.