Pata taarifa kuu

Mwanamuziki nguli Jacob Desvarieux kutoka bendi ya Kassav afariki dunia

Mmoja wa wanamuziki nguli kutoka bendi ya Kassav, katika Visiwa vya Antilles, Jacob Desvarieux, ambaye 'alifanya zouk kutoka ukanda huo kusikika na kutambulika kote ulimwenguni kwa zaidi ya miongo minne na kuweza kupata umaarufu mkuwa alifariki Ijumaa hii, Julai 30 huko Pointe-à-Pitre baaada ya kuambukizwa virusi vya Covid -19. Alikuwa na umri wa miaka 65.

Jacob Desvarieux, 2007.
Jacob Desvarieux, 2007. © RFI / Edmond Sadaka
Matangazo ya kibiashara

Mwanamuziki huyo kutoka Guadeloupe aliyeishi katika jiji kuu la Ufaransa alikuwa na uhusiano wa karibu wa muda mrefu na bara la Afrika na wasanii wake.

Mwanamziki huyu wa mtindo wa Zouk, alikuwa nyota kati bendi yake, lakini pia katika mtindo wa muziki wa taratibu, Zouk, kutokana hasa na sauti yake ya chini lakini yenye uzito wa juu, na jinsi alivyokuwa akiimba.

Jacob Desvarieux alikuwa muimbaji, mpiga gita na mtungaji katika bendi ya Kassav kutoka visiwa vya Antilles.

Kwa zaidi ya miongo minne, akiwa katika bendi ya Kassav ’ambapo alikuwa kiongozi, alibeba bendera ya muziki kutoka Visiwa vya antilles na kuweza kusikika kote ulimwenguni.

Muziki wa Zouk kutoka bendi ya Kassav ulisikika na kupendwa katika nchi nyingi ulimwenguni, hususan Angola, Burkina Faso, Madagascar, Msumbiji, Congo, Cameroon, Senegal, Benin, Côte-d’Ivoire …

"Tuliambiwa kuwa Afrika tulikuwa nyota, lakini hatukuamini. Tulipofika uwanja wa ndege na kuona kwamba kulikuwa na maelfu ya watu wakitungojea, tuliamini ama kweli tuko nyota Afrika," Jacob Desvarieux alisema wakate wa uhai wake, pia akielezea kwamba "ikiwa zouk imefaulu, ni kwa sababu ni mchanganyiko wa muziki wote watu weusi".

Kutokana na umaarufu wake, Jacob Desvarieux aliombwa na kuweza kushirikishwa  kimuziki na wanamuziki maarufu kutoka Afrika: Toofan kutoka (Togo), Yola Araujo (Angola), Patience Dabany (Gabon), Angélique Kidjo (Benin), Alpha Blondy (Côte-d’Ivoire), Manu Dibango (Cameroon), Chébli (Visiwa vya Comoro, Elida Almeida (Cape Verde) ...

Jacob Desvarieux alizaliwa Paris mnamo Novemba 1955.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.