Pata taarifa kuu
UKRAINE

Rais mpya wa Ukraine atoa ahadi ya kumaliza machafuko nchini mwake, saa chache baada ya kula kiapo leo Jumamosi

Rais mpya wa Ukraine anayeungwa mkono na mataifa ya magharibi, Petro Poroshenko, hii leo ameapa Serikali yake kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko ambaye amekula kiapo leo
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko ambaye amekula kiapo leo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Poroshenko anakuwa rais wa 5 kushika nafasi hiyo toka kuundwa kwa taifa la Ukraine lililojitenga kutoka iliyokuwa Jumuiya ya nchi za Kisovieti na sasa Urusi.

Rais Poroshenko amekula kiapo hii loe mjini Kiev, ikiwa ni siku moja tu, toka kiongozi huyo afanye mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza na rais wa Urusi, Vladmir Putin walipokutana nchini Ufaransa siku ya Ijumaa.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko akiwa na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel pamoja na rais wa Urusi, Vladimir Putin walipokutana Ijumaa ya tarehe 6June nchini Ufaransa
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko akiwa na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel pamoja na rais wa Urusi, Vladimir Putin walipokutana Ijumaa ya tarehe 6June nchini Ufaransa Reuters/Kevin Lamarque

Kwenye mazungumzo yake ya hapo jana na rais Putin, rais Porosheko amemueleza wazi wazi kiongozi huyo kutofurahishwa kwake na vitendo vinavyoendelea kushuhudiwa mashariki mwa nchi yake na kumtaka kuongeza ulinzi kwenye maeneo ya mipaka kuzuia wapiganaji zaidi na silaha kuingia nchini humo.

Mbali na kuwa na mazungumzo na rais Putin, rais Poroshenko pia alikuwa na mazungumzo kwa nyakati tofauti na marais wa Marekani Ufaransa, kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameroon.

Poroshenko mwenye umri wa miaka 48 na tajiri aliyejipatia mali zake kupitia biashara kubwa ya Chocolate anayoifanya kwenye nchi yake na ukanda wa Ulaya, saa chache baada ya kuapishwa aliwataka wabunge kusimama kwa dakika moja kuwakumbuka watu 100 waliopoteza maisha toka kuanza kwa machafuko mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Poroshenko amesema kuwa Serikali yake inatangaza msamaha kwa wanaharakati ambao hawajashiriki mauaji ya wananchi mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni hatua yake ya awali aliyoitangaza baada ya kuchukua madaraka kwa lengo la kusitisha mzozo unaoendelea nchini mwake.

Poroshenko anasema kuwa "Nachukua madaraka haya rasmi kwa lengo la kulinda na kuiimarisha umoja ndani ya Ukraine". Alisema rais Poroshenko baada ya kula kiapo.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa "Wananchi wa Ukraine hawataona baraka ya amani na usalama mpaka pale watakapotatua tofauti zao na wenzao wa Urusi".

Poroshenko kwenye hotuba yake akasisitiza kuwa eneo la jimbo la Crimea litabaki kuwa eneo la Ukraine na hilo litafanyika hivi karibuni.

Taarifa toka ikulu ya Duma nchini Urusi, inasema kuw arais Vladmir Putin ameagiza vikosi vyake kwa mara ya kwanza kuimarisha usalama kwenye maeneo yote ya mipaka kati yake na nchi ya Ukraine kwa lengo la kuzuia wapiganaji wenye silaha kuingia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.