Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-UKRAINE-Machafuko

Marekani na Urusi zatuhumiana kufuatia mzozo wa Ukraine

Marekani na Urusi zimelaumiana kuhusu machafauko yanayoshuhudiwa mashariki mwa nchi ya Ukraine baada ya wakaazi wa eneo kudai kura ya maoni ya kujiunga na Moscow. Kiev imeonya kuwa baada ya muda wa mwisho kukamilika waliotoa kwa watu waliojihami kwa silaha wanaominiwa kutoka nchini Urusi kuteka majengo ya serikali, itatumia nguvu kuwaondoa.

Watu wenye silaha mbele ya makao makuu ya polisi,  mjini Slaviansk, aprili 12 mwaka 2014.
Watu wenye silaha mbele ya makao makuu ya polisi, mjini Slaviansk, aprili 12 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Majibizano makali yameshuhudiwa saa chache zilizopita katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huku Marekani kupitia Balozi wake katika umoja wa Mataifa Samantha Power akiituhumu Urusi kuvamia Ukraine kijeshi.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin.
Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin. REUTERS/Eduardo Munoz

Tuhma hizo zimekanushwa vikali na balozi wa Urusi katika Umoja huo wa Mataifa Vitaly Churkin ambaye amesema majeshi ya Urusi yanayodaiwa kuvamia majengo ya serikali yamekuwa eneo hilo kwa muda mrefu yakilinda mpaka wa Urusi.

Mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani yameendelea kuikashifu Urusi kuivamia kijeshi Ukraine na kuonya kuwa itaiwekea vikwazo zaidi vya kiuchumi na kisiasa ikiwa uvamizi huo utaendelea.

Serikali ya Ukraine imeanzisha jana jumapili operesheni ya kuwaondoa katika majengo wanaharakati wanaounga mkono Urusi ambao wameyashikiliya kwa majuma kadhaa, operesheni ambayo serikali imeita”operesheni dhidi ya Ugaidi”.

“Watu wameuawa katika vita vinavyochochewa na Urusi nchini Ukraine”, amethibitisha rais wa mpito wa Ukraine, Olexandre Tourtchinov katika hotuba aliyotoleya wananchi, huku akibaini kwamba ameamuru jeshi kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi ili kukomesha machafuko.

Wakati huohuo serikali ya Urusi imeionya serikali ya Ukraine kusitisha vita dhidi ya raia wake, huku ikiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kuhusu hali hio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.