Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-MAREKANI-Siasa-Uchumi

Marekani yaionya Urusi kutoendelea kuchochea vurugu Ukraine

Urusi imetoa vitisho vya kusitisha kusambaza gesi nchini Ukraine ikihofia kutokea kwa makabiliano kati ya viongozi wa Ukraine na wanaharakati wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine. Rais wa Urusi Vladmir Putin ametahadhari mataifa ya Ulaya kukubali kuilipia Ukraine deni la mabilioni ya fedha, la sivyo ametishia kusitisha kusambaza kwa gesi hio nchini Ukraine.

Hali ya sintofahamu yaendelea kuripotiwa katika mji wa Dontesk.
Hali ya sintofahamu yaendelea kuripotiwa katika mji wa Dontesk. REUTERS/Konstantin Chernichkin
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo, Marekani imeshutumu Urusi kutumia utajiri wake wa gesi kuendelea kuingilia maswala ya Ukraine na kusababisha machafuko nchini humo.

Kauli hii ya Marekani inakuja muda mfupi baada ya Urusi kuyaonya mataifa ya Ulaya kuwa itasitisha kusambaza gesi yake katika mataifa hayo kutokana na deni kubwa ya gesi ambalo linaikabili nchi ya Ukraine.

Marekani na mataifa mengine ya magharibi yametishia kuiwekea vikwazo vya Uchumi nchi ya Urusi ikiwa itaendelea kuchochea maandamano nchini ukraine ambayo sasa yanashuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Marekani Barack Obama ameongea kwa simu na Kansela wa Ujerumani angela Merkel kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi
Rais wa Marekani Barack Obama ameongea kwa simu na Kansela wa Ujerumani angela Merkel kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi REUTERS/Jerry Lampen/Pool

Katika taarifa iliyochapishwa kufuatia mazungumzo kupitia njia ya sim kati ya rais wa Marekani na knsela wa Ujerumani Angela Merkel, Obama amesema kuna umuhimu mataifa ya Ulaya, Marekani na mataifa mengine washirika kujiandaa kuichukulia Urusi vikwazo kwa muda wowote iwapo itaendelea kuchochea vurugu nchini Ukraine.

Hayo yakijiri, hali ya sintofahamu inaendelea kutanda mashariki mwa Ukraine kati ya wanaharakati wanaounga mkono Urusi na wale wanaunga mkono utawala wa Ukraine.

Wakti huohuo viongozi wa Ukraine wamewataka hadi leo ijumaa wanaharakati wanaounga mkono Urusi ambao wanashikilia baadhi ya majengo ya serikali katika mji wa Donetsk kuondoka ndani ya majengo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.