Pata taarifa kuu
UFRANSA-YEMEN-AQPA-USALAMA

Aqpa yadai kufanya mashambulizi dhidi Charlie Hebdo

Katika ujumbe wa video uliyorushwa hewani Jumatano, Januari 14, kundi la al-Qaeda katika Peninsula ya Arabia (Aqpa) limekiri kuhusika katika mauaji yaliyotekelezwa wiki moja iliyopita kwenye makao makuu ya jarida la Charlie Hebdo.

Washambuliaji wakikabiliana na polisi karibu na ofisi ya jarida la kila wiki "Charlie Hebdo".
Washambuliaji wakikabiliana na polisi karibu na ofisi ya jarida la kila wiki "Charlie Hebdo". AFP PHOTO / ANNE GELBARD
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi ambao bado unaendelea, ulithibitisha kwamba kuna uhusiano kati ya ndugu wawili kutoka familia Kouachi na tawi la kundi la al-Qaeda nchini Yemen.

Tangazo hilo la video lililotolewa katika lugha ya Kiarabu na kutafsiriwa kataika lugha ya Kiingereza limewasilishwa katika chumba cha habari cha RFI kisha kusambazwa kwenye intaneti likiwa na maneno yafuatayo : “ Sisi al-Qaeda kutoka Penensula ya Arabia, tunakiri kuhusika katika operesheni iliyokua na lengo la kulipiza kisase dhidi ya kashfa inayotolewa kwa Mtume” Muhammad.

Maneno haya yalisemwa na mmoja wa wakuu wa al Qaeda katika nchi ya Yemen katika Peninsula ya Arabia (Aqpa), Nasser bin Ali al-Anassi. " Mashujaa waliajiriwa na walitekeleza kazi tuliyowatuma", amesema Ali al-Anassi.

Hapa Ali al-Anassi akisema mashujaa alitaka kumaanisha ndugu wawili kutoka familia Kouachi, ambao wahusika katika mauaji ya watu kumi na wawili kwenye makao makuu ya jarida Charlie Hebdo. Ujumbe unasema kuwa shambulio hilo lilifanyika kwa amri ya Ayman al-Zawahiri, kiongozi wa kundi la al Qaeda.

Hotuba hii imetolewa juu ya picha ya mashambulizi na maandamano makubwa ya yaliyofanyika Jumapili Januari 11. Aqpa imerejelea taarifa ya kuwepo kwa marais na viongozi ambao walishiriki maandamano hayo katika mji wa Paris Jumapili Januari 11: " Viongozi wa kikafiri waliumizwa na matukio hayo. hao ndio ambao wanapambana dhidi yetu nchini Afghanistan, Gaza, Syria, Somalia na Yemen".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.