Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAZISHI

Hollande atoa heshima za mwisho kwa polisi waliouawa

Watu waliouawa katika mashambulizi yaliyotokea juma lililopita mjini Paris na vitongoji vyake wamezikwa leo Jumanne Januari 13 mwaka 2015.

Francois Hollande, katika ukumbi wa makao makuu ya polisi ya mjini Paris, Jumanne hii Januari 13 katika sherehe ya kutoa heshima ya mwisho kwa askari polisi watatu waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea juma lililopita.
Francois Hollande, katika ukumbi wa makao makuu ya polisi ya mjini Paris, Jumanne hii Januari 13 katika sherehe ya kutoa heshima ya mwisho kwa askari polisi watatu waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea juma lililopita. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Wayahudi wanne waliouawa katika jumba la biashara wamezikwa leo asubuhi Jerusalem, nchini Israel, na alaasiri amezikwa Ahmed Marabet, askari polisi wa Ufaransa kutoka jamii ya Waislam. Askari polisi huyo ambaye aliuawa katika shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la kila wiki, amezikwa katika kitongoji kimoja cha Paris.

Askari polisi wengine wawili waliuawa katika mashambulizi hayo. Sherehe ya kutoa heshima ya mwisho kwa wahanga hao imefanyika kwenye makao makuu ya polisi mapema Jumanne Janauari 13. Sherehe hiyo imeongozwa na rais wa Ufaransa François Hollande.

Majeneza yaliyokuwemo miili ya askari polisi hao watatu yaliingizwa katika ukumbi wa makao makuu ya polisi, baada ya tarumbeta na ngoma kupigwa.

Majeneza hayo matatu yamekua yamefunikwa bendera ya Ufaransa, huku yakibebwa na askari polisi wanawake kwa wanaume kutoka kitengo cha askari polisi hao waliouawa. Wimbo wa taifa la Ufaransa " La marseillaise" umesikika wakati majeneza hayo yalipokua yakinyanyuliwa.

Rais wa Ufaransa amekagua kikosi cha askari polisi waliokua wamekuja kushiriki katika sherehe hiyo. Walioshiriki sherehe hiyo wamesalia kimya kwa muda wa dakika kumi. Kisha rais Hollande amechukua nafasi ya kutoa heshima ya mwisho kwa maafisa watatu wa polisi waliouawa.

" Nchi yetu kubwa, nzuri, kamwe haitojidhalilisha,kamwe haitokubali vitisho, wala kunyenyekea kwa watu wasioeleweka. Ufaransa iko imara na itaendelea kuwajibika kwa kulinda raia wake", amesema rais Hollande.

Ahmed Merabet, ambaye ni kutoka jamii ya Waislam, amezikwa katika makaburi ya Waislam ya Bobigny.

Askari polisi wengine wawili waliuawa katika mashambulizi ya kigaidi. Franck Brinsolaro, alikua akitoa ulinzi kwa mhariri wa jarida la kila wiki la Charlie Hebdo, Charb. Aliuawa wakati wa shambulio dhidi ya jarida hilo la vibonzo.

Clarissa Jean-Philippe, askari polisi mwanamke, mwenye umri wa miaka 27, aliuawa katika kitongoji cha Montrouge na Amédy Coulibaly Alhamisi Januari 8 mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.