Pata taarifa kuu
USALAMA BAHARINI

Uhamaji: Watano wafariki wakati wa jaribio la kuvuka Manche

Takriban wahamiaji watano, ikiwa ni pamoja na mtoto mmoja, wamefariki baada ya "umati wa watu" wakisafiri baharini wakati wa jaribio la kuvuka Bahari ya Mache usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne kutoka pwani ya kaskazini mwa Ufaransa.

Angalau wahamiaji watano, ikiwa ni pamoja na mtoto mmoja, wamefariki wakati wakijaribu kuvuka Bahari ya Manche (picha ya kielelezo).
Angalau wahamiaji watano, ikiwa ni pamoja na mtoto mmoja, wamefariki wakati wakijaribu kuvuka Bahari ya Manche (picha ya kielelezo). AFP - BERNARD BARRON
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea saa 11:00 asubuhi, kaskazini mwa Ufaransa, wakati boti ndogo lililokuwa na zaidi ya watu 110 ilisafiri baharini kutoka ufuo wa Wimereux, kulingana na Halmashauri ya wilaya hiyo. "Baada ya kukwama kwa mara ya kwanza kwenye ukingo wa mchanga, mashua ilisafiri tena," Malaka hiyo imesema. "Umati wa watu ulionekana katika boti iliyojaa kupita kiasi, na kusababisha waathiriwa kadhaa. "

Jaribio la kuvuka lilifanyika kwenye bahari tulivu na hali ya hewa safi, lakini kwa hali ya joto karibu digrii chache juu ya sifuri.

Vifo kumi na mbili mnamo 2023

Mkasa wa mwisho ulitokea Machi 3 na kifo cha mtoto wa miaka saba kuzama kwenye mfereji wa Aa, mto mdogo katika eneo hilo unaoingia Bahari ya Kaskazini, wakati akiwa kwenye boti ndogo na wahamiaji wengine 15.

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, Turk mwenye umri wa miaka 22 alifariki baada ya kuanguka kutoka kwa boti karibu na pwani ya Calais na wahamiaji wengine wawili kutoweka. Raia mmoja wa Eritrea alifunguliwa mashtaka na kufungwa jela siku ya Jumamosi katika kesi hii. Usiku wa Januari 13 kuamkia Januari 14, wahamiaji watano, ikiwa ni pamoja na kijana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Syria, walifariki huko Wimereux wakati wakijaribu kufikia boti ambalo lilikuwa baharini ndani ya maji ya nyuzi 9.

Wahamiaji 12 walipoteza maisha mwaka wa 2023 walipokuwa wakijaribu kuvuka Mache, kulingana na mamlaka. Mwaka huo huo, wahamiaji 29,437 walifika ufuo wa Uingereza kinyume cha sheria, ikilinganishwa na 45,774 mwaka 2022, mwaka wa rekodi, kulingana na takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.