Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Jeshi la Kyiv ladai kudungua ndege ya kijeshi ya Urusi kwa mara ya kwanza

Jeshi la wanahewa la Ukraine limetangaza leo Ijumaa Aprili 19 kwamba limedundua ndege muhimu ya aina yake ya kijeshi ya Urusi, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi ulioanzishwa na Moscow. Urusi, kwa upande wake, inataja kifo cha mmoja wa mfanyakazi katika ajali ya ndege kufuatia "kasoro za kiufundi", bila kutaja ikiwa ni ndege hiyo inayodaiwa kudondoshwa.

Ndege ya kivita ya Urusi aina ya Tu-22M3 ilianguka katika jimbo la Stavropol mnamo Ijumaa Aprili 19, 2024. Jeshi la Ukraine linadai kuwa imeidungua.
Ndege ya kivita ya Urusi aina ya Tu-22M3 ilianguka katika jimbo la Stavropol mnamo Ijumaa Aprili 19, 2024. Jeshi la Ukraine linadai kuwa imeidungua. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Kwa mara ya kwanza, vitengo vya kombora vya kupambana na ndege vya Jeshi la Anga, na kwa kushirikiana na idara ya upelelezi katika ulinzi wa Ukraine, vimeharibu ndege ya kimkakati ya kivita ya kurusha makombora ya masafa marefu aina ya Tu-22M3, ikiwa imebeba makombora ya X-22 yanayotumiwa na magaidi wa Urusi kushambulia miji yenye amani ya Ukraine,” Kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Ukraine Mikola Oleshchuk amesema kwenye Telegram.

Kulingana na idara ya ujasusi wa jeshi la Ukraine (GUR), ndege ya Urusi "ilidunguliwa kutokana na operesheni maalum iliyofanywa na ujasusi wa ulinzi wa Ukraine kwa ushirikiano na Jeshi la Wanahewa." Athari angani ilifanyika "kwa umbali wa takriban kilomita 300 kutoka Ukraine", inaongeza GUR, ambayo inabainisha kuwa ndege hiyo iliweza kuruka hadi eneo la Stavropol "ambapo ilianguka ".

Kwa upande wa Urusi, habari hi haijathibitishwa. Wizara ya Ulinzi haijathibitisha shambulio la Ukraine dhidi ya ndege yake. Hata hivyo, chanzo katika jeshi la Moscow kimeliambia shirika la habari la serikali TASS kwamba ndege ya kivita aina ya Tupolev-22M3 "ilianguka katika eneo la Stavropol baada ya misheni ya mapigano, wakati kirejea kwenye kambi yake.

Vladimir Vladimirov, gavana wa jimbo la Stavropol, amebaini kwenye Telegram kwamba ndege ya Tupolev-22M3 ilipata ajali, na kwamba "kulingana na data ya awali, kasoro za kiufundi ndizo sababu ya ajali." Mfanyakazi mmoja amefariki, wengine wawili walipatikana wakiwa hai na waokoaji bado wanamtafuta wa nne, gavana ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.