Pata taarifa kuu

Ukraine: Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi matatu ya Urusi huko Chernihiv

Takriban watu kumi na watatu wameuawa katika mashambulizi matatu ya Urusi siku ya Jumatano huko Chernihiv, mji mkubwa kaskazini mwa Ukraine. Rais Volodymyr Zelensky kwa mara nyingine tena amelaumu ukosefu wa misaada kutoka nchi za Magharibi.

Waokoaji wakifanya kazi katika eneo la hoteli iliyoharibiwa katika shambulio la kombora la Urusi huko Chernihiv, Ukraine, Aprili 17, 2024.
Waokoaji wakifanya kazi katika eneo la hoteli iliyoharibiwa katika shambulio la kombora la Urusi huko Chernihiv, Ukraine, Aprili 17, 2024. © REUTERS - Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limesababisha "vifo vya watu kumi na watatu na 60 kujeruhiwa kufikia hatua hii," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Igor Klimenko amesema. Idadi ya vifo inaweza kuongezeka, na "angalau" watu watatu hawajulikani waliko na operesheni ya kuwatafuta bado inaendelea. Huko Chernihiv, "milipuko mitatu ilitokea" saa 9:03 asubuhi kwa saa za ndani, Meya Oleksandr Lomako alibainisha mapema siku hiyo kwenye televisheni.Yalikuwa "mashambulizi ya moja kwa moja kwenye jengo la miundombinu ya kijamii".

Wizara ya Afya ya Ukraine imesema kituo cha afya kimeharibiwa. Watu sita walilazwa hospitalini, aimeongeza kwenye Telegram. Gavana wa jimbo ambalo Chernihiv ndio mji mkuu wake amebaini kwamba mashambulio hayo yameathiri katikati mwa jiji.

Moja ya miji kongwe nchini Ukraine, iliyoanzishwa zaidi ya miaka 1,000 iliyopita, Chernihiv, ilikuwa na karibu wakaazi 300,000 kabla ya uvamizi wa Urusi mnamo mwezi wa Februari 2024. Unapatikana karibu kilomita sitini kutoka mpaka wa Belarusi - mshirika waUrusi, na karibu kilomita mia kadhaa  kutoka Kiev, Chernihiv ilishambuliwa vikali na jeshi la Urusi mwanzoni mwa mashambulizi haya. Sehemu ya mkoa wake ilikuwa imekaliwa kwa wiki kadhaa.

"Hii haingefanyika ikiwa Ukraine ingepokea vifaa vya kutosha"

Rais Volodymyr Zelensky amesema Ukraine haikuwa na ulinzi wa kutosha wa anga ili kuzuia shambulio hili, moja ya mauaji mabaya zaidi dhidi ya jiji hili. "Hili lisingetokea kama Ukraine ingepokea vifaa vya kutosha vya ulinzi wa anga na kama dhamira ya dunia ya kupinga ugaidi wa Urusi ingetosha," kiongozi wa Ukraine amesisitiza kwenye Telegram. Urusi hushambulia miji ya Ukraine kila siku kwa makombora na droni zinazolipuka, pamoja na miundombinu yake ya nishati.

Kutokana na misaada ya nchi za Magharibi, hasa misaada kutoka Marekani, ambayo imesitiswa, Ukraine inakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kuzuia vifaa hivi. Inawahimiza washirika wake kuwasilisha silaha zaidi na mifumo ya ulinzi wa anga.

Kusitasita kwa washirika kumefadhaisha sana Kyiv baada ya shambulio la anga la Iran dhidi ya Israeli mwishoni mwa wiki hii, shambulio ambalo lilizimwa kwa mafanikio, haswa kutokana na msaada wa kijeshi wa nchi za Magharibi, wakati msaada muhimu wa Marekani umezuiwa kwa miezi kadhaa kwenye Bunge la Congress.

Rais Zelensky kwa hivyo ametoa mfano wa kituo kikubwa cha nguvu za mafuta karibu na Kyiv, kilichoharibiwa kabisa na makombora ya Urusi mnamo Aprili 11, kwa sababu, kulingana na yeye, na ukosefu wa risasi kwa ulinzi wa kupambana na ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.