Pata taarifa kuu

Uswisi kuandaa Kongamano kuhusu Amani nchini Ukraine mnamo Juni 15 na 16

Kwa kuzingatia Mkutano wa Amani nchini Ukraine ambao Uswisi unapanga kuandaa mnamo Juni 15 na 16, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametaja kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba China inaweza kusaidia "kuharakisha" amani.

Wanajeshi wa Ukrainei wa kikosi cha 58 wakifanya mazoezi kwenye safu ya ufyatuaji risasi katika eneo la Donetsk, huku kukiwa na shambulio la Urusi nchini Ukraine, Aprili 7, 2024.
Wanajeshi wa Ukrainei wa kikosi cha 58 wakifanya mazoezi kwenye safu ya ufyatuaji risasi katika eneo la Donetsk, huku kukiwa na shambulio la Urusi nchini Ukraine, Aprili 7, 2024. REUTERS - Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky ameonya kwamba kipaumbele lazima kiwe "kurejesha heshima kamili kwa malengo na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na kuheshimu kanuni za uadilifu wa eneo". Njia ya kutaka kuachiliwa kwa maeneo ya Ukraine yanayodhibitiwa kwa manufaa ya Moscow.

Kauli hii inakuja baada ya mkutano wa Beijing siku ya Jumanne kati ya Olaf Scholz na Xi Jinping. Kansela wa Ujerumani alisema alimwomba rais wa China kuishinikiza Moscow kuacha "kampeni yake isiyo na maana" nchini Ukraine. "Neno la China lina uzito nchini Urusi," alisema.

Kansela wa Ujerumani pia alitangaza kwamba "China na Ujerumani zinataka kushauriana kwa dhati na kwa njia chanya juu ya kukuza kuandaliwa kwa mkutano wa ngazi ya juu nchini Uswisi na mikutano ya kimataifa ya baadaye ya amani." Olaf Scholz amesisitiza sana haja ya kuzidisha juhudi za kidiplomasia kujaribu kutafuta suluhu la vita vya Ukraine, huku Ujerumani hadi sasa ikilenga zaidi misaada ya kijeshi kwa Kyiv.

China imesema Jumatano kwamba bado kulikuwa na "kazi nyingi ya kufanya" kabla ya uwezekano wa kufanyika kwa mkutano huu nchini Uswisi kuhusu Ukraine.

Katika mkutano wake na Olaf Scholz, Xi Jinping alisema China "inaunga mkono kuitishwa kwa wakati kwa mkutano wa kimataifa wa amani unaotambuliwa na Urusi na Ukraine, kwa ushiriki sawa wa pande zote na majadiliano ya haki ya mipango yote ya amani," Lin Jian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, imesema siku ya Jumatano.

Maoni haya yanabainisha kuwa China haiungi mkono kufanyika kwa mkutano huu nchini Uswisi katika hali ya sasa, kwani Urusi haitashiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.