Pata taarifa kuu

Wanachama wa EU waahidi silaha za kuzuia mashambulizi ya anga kwa Kyiv na kuiwekea vikwazo Iran

Wakuu wa nchi na serikali wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya wanakutana katika mkutano wa kilele mjini Brussels. Mgogoro wa Mashariki ya Kati umechukua sehemu kubwa yamazungumzo ya viongozi wa Ulaya mnamo Jumatano usiku Aprili 17.

Charles Michel huko Kyiv mnamo Novemba 21, 2023.
Charles Michel huko Kyiv mnamo Novemba 21, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Brussels, Julien Chavanne

Huko Kyiv, Volodymyr Zelensky ana hisia ya kuchukuliwa kuwa mshirika wa kiwango cha pili baada ya kuungwa mkono na Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa Israel, huku jeshi la Urusi likisonga mbele kuelekea upande wa mashariki. Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya hatimaye wamejitolea kwa mara nyingine tena kuharakisha usafirishaji wa silaha.

Hivi ndivyo Volodymyr Zelensky alitaka kusikia. Shinikizo lake linaonekana kuzaa matunda tangu Umoja wa Ulaya ulipojitolea, Jumatano Aprili 17, kuwasilisha silaha za kuzuia mashambulizi ya anga kwa Kyiv haraka iwezekanavyo.

"Hakuna wakati tena wa maneno mengi, tunahitaji silaha zaidi," amebainisha Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya. Tulikuwa na majadiliano mazuri na tulielewa kuwa nchi wanachama, hasa zile zilizo na uwezo wa uzalishaji, zinajua kwamba ni muhimu sana kutoa mifumo zaidi ya ulinzi dhidi ya ndege na risasi zaidi. "

Rais wa Ukraine aliweza kutegemea uungwaji mkono mkubwa wa nchi kadhaa za Ulaya: Uholanzi, lakini pia Lithuania na rais wake Gitanas Nauseda: "Ninaogopa kwamba tunapoteza mtazamo wa Ukraine. Kila siku na kila usiku, miji ya Ukraine inashambuliwa kwa mabomu, "amesema.

Kansela wa Ujurumani Olaf Scholz anatoa wito kwa wenzake kufuata mfano wake: kutoa mifumo ya ulinzi ya Patriot. "Ni muhimu mara moja kwa Ukraine na tunataka kuwahimiza wengine kufanya hivyo. Siku ya Jumamosi Berlin ilitangaza kutumwa kwa mfumo huu wa Patriot kusaidia Ukraine kukabiliana na mashambulizi ya Urusi yanayolenga miji yake na miundombinu ya nishati, ambayo imeongezeka katika wiki za hivi karibuni. Huu ni mfumo wa tatu wa Patriot ambao Berlin imetoa kwa Kyiv. “Asante Olaf, kwa ufanisi wako. Hata hivyo, tunahitaji zaidi, "amesema, akisisitiza kwamba shambulio la Jumatano kwenye mji wa Chernihiv wa Ukraine, ambalo lilisababisha vifo vya watu 17, lilionyesha udharura wa hali hiyo.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, kwa upande wake, siku ya Jumatano alihimiza nchi za Muungano wa Atlantiki kutumia hisa zao kwa ajili ya Ukraine, hata kama hii itawaweka chini ya kiwango kilichopendekezwa na NATO.

Kwa hivyo Volodymyr Zelensky amepata ahadi mpya kutoka kwa washirika wake wa Ulaya. Inabakia, kwa mara nyingine tena, kuwasilisha haraka iwezekanavyo kutokana na kwamba jeshi la Urusi linaendelea kusonga mbele.

EU yaziwekea vikwazo kampuni zinazotengeneza makombora na ndege zisizo na rubani zaIran

Hata hivyo, Umoja wa Ulaya umeamua Jumatano usiku kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran vinavyolenga kampuni zinazotengeneza ndege zisizo na rubani na makombora, ametangaza Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel. "Tumeamua kuweka vikwazo dhidi ya Iran, tulitaka kutuma ujumbe wazi" baada ya shambulio la Israel, ametangaza baada ya mkutano huo. "Tulikuwa na majadiliano mazuri na tunafikiri kwamba ni muhimu sana kufanya kila kitu ili kuitenga Iran, kufanya kazi na nchi za kanda ili kuhakikisha kwamba tunaunga mkono mchakato wa amani, mazungumzo ya amani. Tunaunga mkono usalama wa Israeli, bila kusita. Na tunasadikisha kuwa ni muhimu sana kushirikiana na nchi katika eneo hili ili kuepusha mivutano zaidi, ambayo ni kuongezeka kwa uhasama. Ni lazima tuzuie kuongezeka uhasama kuenea katika kanda," amesema, na kuongeza: "wazo ni kulenga makampuni ambayo yana jukumu katika kutengeneza droni na makombora. "

Katika tamko lao lililopitishwa mwishoni mwa mkutano huo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatoa wito kwa "wahusika wote kujizuia zaidi na kujiepusha na kitendo chochote ambacho kinaweza kuongeza mvutano katika eneo hilo". Iran ilirusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel usiku kucha kuanzia Jumamosi hadi Jumapili, kujibu shambulio la Aprili 1 kwenye ubalozi wa Iran mjini Damascus, Syria, unaohusishwa na Israel. Takriban makombora na ndege zisizo na rubani ziliharibiwa kabla ya kuanguka nchini Israel. Hili lilikuwa shambulio la kwanza la moja kwa moja la Iran dhidi ya Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.