Pata taarifa kuu

Guadeloupe: Sheria ya kutotoka nje usiku kwa watoto yatangazwa Pointe-à-Pitre

Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin ametangaza hivi punde Jumatano usiku sheria ya kutotoka nje usiku kwa kipindi cha miezi miwili kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 18 huko Pointe-à-Pitre ili kukpambana na kuzuka kwa uhalifu katika wilaya wa Guadeloupe.

Kulingana na Halmashauri ya wilaya ya Guadeloupe, visiwa hivyo vina mauaji mara sita zaidi, majaribio ya mauaji mara tisa na wizi wa kutumia silaha mara 20 zaidi ya wastani wa kitaifa.
Kulingana na Halmashauri ya wilaya ya Guadeloupe, visiwa hivyo vina mauaji mara sita zaidi, majaribio ya mauaji mara tisa na wizi wa kutumia silaha mara 20 zaidi ya wastani wa kitaifa. AFP - CEDRICK-ISHAM CALVADOS
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Machi, meya wa Pointe-à-Pitre Harri Durimel (EELV) alielezea jiji hilo kama "jinamizi la hali nzito", ambapo "hali inatisha". Akiwa ziarani huko Guadeloupe, Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin kwa hivyo aliagiza Jumatano usiku kutangazwa kwa sheria ya kutotoka nje ya miezi miwili kwa wale walio chini ya umri wa miaka 18 katika jaribio la kukomesha hali hiyo jijini. Hatua hiyo "itatumika kuanzia mwanzoni mwa wiki ijayo" ili kupambana dhidi ya "uhalifu ambao [...] unazidi kukuwa, ukiambatanishwa na silaha zinazoendelea kuenea," amesema Gérald Darmanin wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Pointe-à-Pitre, ambapo anazuru. Hatua hii itatumika kwa usahihi usiku kuanzia saa 2. "Hatuwezi kuruhusu watoto wa miaka 12, 13, 14, kutembea na silaha, kuzunguka saa 4 usiku mitaani, kushambulia maafisa wa polisi, kushambulia watalii, kushambulia wapita njia," ameongeza.

Meya Harry Durimel, aliyechaguliwa tangu mwaka 2020, amekaribisha tangazo la Waziri wa Mambo ya Ndani lililotolewa baada ya mkutano na Mjumbe wa Waziri wa Maeneo ya Ng'ambo Marie Guévenoux, gavana na yeye mwenyewe. "Hiki ni kitu muhimu," amejibu. "Hapo awali, ilikuwa ni 12% ya watoto wanaofanya uhalifu na sasa ni 38% ya vitendo vya uhalifu," ameongeza. "Kama watoto wako nyumbani kwa wazazi wao usiku, hawatachoma mikebe 70 ya takataka kama walivyofanya huko Pointe-à-Pitre wiki iliyopita," amebainisha.

Mnamo Machi 24, katika muktadha wa vurugu za mijini na mfululizo wa vitendo vya unyanyasaji kwa kutumia silaha, wakati mwingine mbaya, alitishia kujiuzulu. "Nina hisia kwamba kilio nilichotoa wiki chache zilizopita kimesikika," alitangaza kwa shirika la habari la AFP, akimaanisha uwezekano wa "kuifanya Pointe-à-Pitre eneo dogo la kilomita mraba 2.6, maabara ya usalama wa jamhuri" .

"Shughuli za usawa wa jumla"

Kulingana na halmashauri ya wilaya ya Guadeloupe, visiwa hivyo vina "mauaji mara sita zaidi, mara tisa zaidi ya majaribio ya mauaji - nusu kwa kutumia bunduki - na mara 20 zaidi ya wizi wa kutumia silaha kuliko wastani wa kitaifa". Katika miezi ya hivi majuzi, Pointe-à-Pitre - iliyo kuwa na wakaazi 14,500 mnamo mwaka 2020 - imeshuhudia matukio makubwa ya historia. Mnamo mwezi Machi, mfanyabiasaha aliuawa katika wilaya hiyo katika tukio la wizi wa kutumia bunduki. Watalii waliokuwa kwenye meli walidungwa kisu na mwanamke aliyekuwa na matatizo ya akili.

Msururu wa hatua za kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu utaambatana na sheriaya kutotoka nje. Kwa hivyo Gérald Darmanin ametangaza kwa mwezi ujao "operesheni za vita dhidi ya dawa za kulevya, dhidi ya vituo vya uuzaji wa dawa za kulevya na usambazaji wa silaha, hali ambayo bila shaka ndio shida kuu inayoikabili Guadeloupe leo".

"Mkataba mpya wa usalama huko Guadeloupe" pia utawekwa, kama ilivyofanyika Martinique na "ambayo inafanya kazi vizuri, ambayo imepunguza uhalifu", kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa.

Waziri pia alizungumzia "ushirikiano wa kimataifa" na visiwa jirani vya Saint Lucia na Dominica "kupambana dhidi ya uhamiaji haraùu, usambazaji wa silaha, na biashara ya madawa ya kulevya". Pia ametangaza kuwepo kwa "kamera zaidi za ulinzi wa video", zilizounganishwa "na vituo vya usimamizi wa polisi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.