Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UGIRIKI-DIPLOMASIA-UCHUMI

Ujerumani yaisihi Ugiriki

Ujerumani imeionya serikali mpya ya Ugiriki kuhakikisha kuwa inazingiatia masharti ya wakopaji ambao wamekuwa wakisaidia kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel akiisihi Ugiriki kuhakikisha kuwa inazingiatia masharti ya wakopaji ambao wamekuwa wakisaidia kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel akiisihi Ugiriki kuhakikisha kuwa inazingiatia masharti ya wakopaji ambao wamekuwa wakisaidia kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffan Seibert amesema ni muhimu kwa serikali hiyo kuhakikisha kuwa masharti hayo yanazingatiwa ili kuendelea na juhudi za uimarishwaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Tayari Alexis Tsipras ameapishwa kuwa Waziri mkuu baada ya chama chake cha Syriza kushinda uchaguzi wa Wabunge mwishoni mwa juma lililopita.

Chama cha Syriza kimekuwa kikisema hakiamini katika sera ya kubana matumizi ya fedha kama ilivyoshuhudiwa katika serikali zilizopita.

Chama hicho cha Syriza kimekua kikipinga hatua ya kubana matumizi nchini Ugiriki. Kiongozi wa chama cha Syriza, Alexis Tsipras, amewaambia wafuasi wake katika mji mkuu wa Ugiriki, Anthens kuwa hatua ya kubana matumizi iliyotangazwa na serikali inayoondoka madarakani, imefikia mwisho na watafanya kazi na wakopeshaji na kukubaliana namna ya kushughulikia madeni ya taifa.

Waziri mkuu anayeondoka madarakani Antonis Samaras alimtaka hivi karibuni kiongozi wa chama cha Syriza Alexis Tsipras kumpongeza. Samaras alidai kuwa sera zake zilisaidia kufufua uchumi wa Ugiriki na kwamba walichukua hatua kudumisha hali ya usalama wa raia. Amesema kuwa anakabidhi nchi ambayo ni mwanachama wa umoja wa Ulaya na sarafu ya euro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.