Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-UFARANSA-URUSI-CHINA-UJERUMANI-UINGEREZA-NYUKLIA-DIPLOMASIA

Iran: John Kerry atoa wito wa kuhitimisha mazungumzo

Mazungumzo kati ya nchi sita zenye nguvu duniani na Iran yako njia panda, amesema waziri wa mambo ya nje wa Markani John Kerry, kutoka Austria ambapo mazungumzo haya yanafanyika.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, mjini Vienna, Julai 5 mwaka 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, mjini Vienna, Julai 5 mwaka 2015. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amejiunga katika mji wa Vienna na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi zenye nguvu duniani ikiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Iran.

Mawaziri wote hao wamekubaliana kukimbizana na muda. Mpaka usiku wa manane wa Jumanne wiki hii, makubaliano yatakua yametiliwa saini.

" Ni matumaini yetu kuwa mkataba wa haki (...) utapatikana na kuonyesha dunia kuwa nchi zinaweza kukubaliana, lakini bado hatujafikia hatua hiyo na natilia mkazo hatua hii: bado tuna masuala magumu ya kutatufutia suluhu, na tunapaswa kuwajibika kama tulivyosema kabla ya tarehe ya mwisho ya Julai 7 mwaka huu ", amesema John Kerry.

John Kerry, au waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, ambaye aliwasili Jumapili jioni katika mji wa Vienna, wamesema masuala yote yamewekwa mezani. Maamuzi yanapaswa kuchakuliwa ili kukomesha hali hii ya mpango wa nyuklia wa IranI, ambao unaonekana kuleta athari katika mahusiano ya kimataifa tangu mwaka 2003.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.