Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Ufaransa: makabiliano yatokea kati ya polisi na watu wenye silaha Saint-Denis

Kumekuwa na makabiliano makali kati ya polisi wa Ufaransa na watu wenye silaha Kaskazini mwa jiji la Paris alfajiri leo Jumatano.

Wachunguzi wa Ufaransa katika mtaa wa eneo la Saint-Denis, kaskazini mwa Paris, baada ya milio ya risasi ambapo askari polisi mmoja alijeruhiwa, Oktooba 5, 2015.
Wachunguzi wa Ufaransa katika mtaa wa eneo la Saint-Denis, kaskazini mwa Paris, baada ya milio ya risasi ambapo askari polisi mmoja alijeruhiwa, Oktooba 5, 2015. AFP PHOTO / THOMAS SAMSON
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa polisi walivamia eneo la Saint-Denis linaloaminiwa kuwa baadhi ya washukiwa wa kigaidi wanajificha. Baadhi ya askari polisi wamejeruhiwa

Haya yanajiri, wakati maafisa wa usalama nchini humo wakibaini mshukiwa wa tisa wa mashambulizi ya jijini Paris wiki iliyopita yaliyosababisha vifo vya zaidi yawatu 129.

Kamera ya usalama zimemwonesha mtu huyo wa tisa akiwa anasafarisha kundi la watu wanaoaminiwa kutekeleza mashambulizi hayo katika hoteli na baa mbalibali jijini Paris.

Haijafahamika vema ikiwa mshukiwa huyo mpya ni yule anayezuiliwa nchini Ubelgiji au bado hajakamatwa.

Kutoka na shambulizi hilo la Paris usalama umeimarishwa katika mataifa mbalimbali ya Ulaya na mchuano wa kirafiki kati ya Ujerumani na Uholanzi uliotarajiwa kuchezwa Jumanne wiki hii ulisitishwa kwa hofu ya usalama.

Ufaransa na mataifa mengine ya Magharibi yamesisitiza kuwa yatafanya kile kilicho ndani ya uwezo wao wa kupambana na ugaidu duniani.

Kundi la Islamic State lilidai kutekeleza mashambulizi hayo ya Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.