Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UHAMIAJI-USALAMA

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ajiuzulu

Hasira ya wazalendo juu ya mvutano kuhusu uhamiaji umeiangusha serikali ya Ubelgiji na kumlazimu waziri mkuu Charles Michel kutangaza kujiuzulu.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michels, hapa akiwa Brussels  tarehe 14 Desemba, amewasilisha barua ya kuiuzulu kwa Mfalme Philippe tarehe 18 Desemba 2018.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michels, hapa akiwa Brussels tarehe 14 Desemba, amewasilisha barua ya kuiuzulu kwa Mfalme Philippe tarehe 18 Desemba 2018. REUTERS/Piroschka Van De Wouw
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa imesalia miezi mitano tu kabla ya kufanyika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Mei haikuweza kubainika ikiwa mfalme Philippe angeridhia uamuzi wa ghalfa wa Michel.

Taarifa ya ikulu imesema bado uamuzi unasubiriwa ingawa chanzo kimoja kimesema huenda utawala wa kifalme utaitaka serikali ya Michel kusimamia shughuli za kila siku za serikali hadi pale kalenda ya uchaguzi itakapo tajwa.

Siku ya Jumapili katika mjadala wa bungeni, waziri mkuu huyo, Mliberali alikitri kushindwa kukabiliana na kura ya kutokuwa na imani ambayo iliitishwa na vyama vya mrengo wa kushoto na upinzani.

Michel, ambaye aliingia madarakani mnamo 2014 alipoteza uungwaji mkono na chama chake (N-VA) kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa uhamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.