Pata taarifa kuu
UINGEREZA-HAKI

WikiLeaks: Julian Assange aruhusiwa kukata rufaa nchini Uingereza

Mahakama nchini Uingereza imemruhusu muasisi wa mtandao wa kufichua siri wa WikiLeaks, Julian Assange, kupinga uamuzi wa mahakama ulioidhinisha kurejeshwa kwake nchini Marekani.

Mahakama Kuu mjini London imemruhusu mwasisi wa WikiLeaks, Julian Assange kupinga katika Mahakama ya Juu ya Uingereza uamuzi wa mahakama unaoidhinisha kurejeshwa kwake nchini Marekani
Mahakama Kuu mjini London imemruhusu mwasisi wa WikiLeaks, Julian Assange kupinga katika Mahakama ya Juu ya Uingereza uamuzi wa mahakama unaoidhinisha kurejeshwa kwake nchini Marekani Justin TALLIS AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Desemba 10, Mahakama Kuu ya London iliamua kwamba Julian Assange anaweza kurejeshwa Marekani. Alikuwa amebaini kwamba hana imani na ahadi ya marekani juu ya mazingira ya kuzuiliwa kwake nchini Marekani.

Mahakama Kuu mjini London iliamua Januari 24 kumruhusu Julian Assange kupinga kurejeshwa kwake. Mwezi Desemba 2021, mahakama hiyo ilibatilisha rufaa kukataa kumrejesha Marekani raia huyo wa Australia, mwenye umri wa miaka 50, nchini Marekani na na kuchukuwa uamzi wa kurejesha  nchini Marekani kwa kuzingatia kwamba dhamana ya maandishi iliyokuwa imetolewa na mamlaka ya Marekani kuhusiana na mazingira ya kizuizini kwa mtuhumiwa. Marekani pia ilikuwa imebaini uwezekano kwamba anaweza kuomba kutumikia kifungo chake nchini Australia.

Uamuzi wa leo ni ushindi kwa mwasisi wa Wikileaks ambaye, kama mahakma ingelikataa, angelitakiwa kuondoka ndani ya siku 28 kwenda Marekani. "Sina maneno ya kusema jinsi nilivyofarijika," amejibu Sue Barnett, 61, akihojiwa na shirika la habari la AFP mbele ya Mahakama Kuu huko London.

Stella Morris, mchumba wake, amesema: “Kilichotokea mahakamani ndicho tulichotarajia. Lakini hatusahau kwamba hadi kesi hii ifutwe, Julian anaendelea kuteseka… Vita vyetu vinaendelea na tutaendelea hadi kuachiliwa kwake, "amesema mwandishi wa RFI huko London, Marie Boëda.

Julian Assange, raia wa Australia mwasisi wa WikiLeaks, anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 175 jela kwa kuruhusu kusambazwa kwa hati za siri zaidi ya 700,000 kuhusu shughuli za kijeshi za Marekani, hasa nchini Iraq na Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.