Pata taarifa kuu

Vladimir Putin azindua 'operesheni ya kijeshi' nchini Ukraine, milipuko yaripotiwa Kiev

Katika hotuba ambayo haikutangazwa kwenye televisheni mapema Alhamisi, rais wa Urusi alitangaza kwamba ameidhinisha operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa Ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Februari 21, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa Ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Februari 21, 2022. © ALEXEY NIKOLSKY / SPUTNIK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha ametoa wito kwa wanajeshi wa Ukraine kuweka chini silaha zao na kuahidi kulipiza kisasi dhidi ya wale wanaoingilia operesheni ya Urusi nchini Ukraine.

Wakati huo huo, milipuko iliripotiwa katikati mwa Kiev, mji mkuu wa Ukraine, lakini pia katika miji kadhaa ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza Alhamisi Februari 24 operesheni ya kijeshi nchini Ukraine kuwatetea wanaotaka kujitenga mashariki mwa nchi hiyo. "Nilifanya uamuzi kwa ajili ya operesheni maalum ya kijeshi," alisema katika taarifa ya iliyoshangaza wengi kwenye televisheni muda mfupi kabla ya saa 3 asubuhi saa za kimataifa, kwa mara nyingine tena kushutumu "mauaji ya kimbari" yaliyopangwa na Ukraine mashariki mwa nchi, akitaja wito wa msaada kutoka wanaotaka kujitenga uliotangazwa usiku na sera ya uchokozi ya NATO dhidi ya Urusi, ambayo Ukraine ndio chombo chake.

Aliwahutubia askari wa Ukraine akiwaambia: "Ninawaomba muweke chini silaha zao", akiwataka "kuondoka kwenye uwanja wa vita bila kizuizi". Alihakikisha kwamba hana lengo "kukalia" kimabavu Ukraine, lakini "kupokonya silaha jeshi lake.

"Nina hakika kwamba askari na maafisa wa Urusi watatimiza wajibu wao kwa ujasiri," alisema tena, "usalama wa nchi umehakikishwa".

Hakutoa maelezo yoyote kuhusu ukubwa wa operesheni hiyo ya kijeshi, iwapo itafanyika mashariki mwa Ukraine au ikiwa itakuwa pana zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.