Pata taarifa kuu

Mashirika manne yatangaza kuishtaki Denmark kwa mauzo yake ya silaha kwa Israel

Mashirika manne yasiyo ya kiserikali yametangaza siku ya Jumanne Machi 12 kwamba yameishitaki Denmark ili kuilazimisha kusitisha uuzaji wa silaha zake kwa Israel.

Malalamiko hayo ni mwendelezo wa mahakama ya Uholanzi ambayo iliagiza Uholanzi katikati ya mwezi wa Februari kusitisha usafirishaji wa sehemu za F-35 kwenda Israel. Ndege mbili za kivita za F-35 zimepigwa picha kwenye kambi ya kikosi cha wanaanga cha Royal Danish Air Force (RDAF) Fighter Wing Skrydstrup, Denmark, Oktoba 1, 2023 (Picha ya kielelezo).
Malalamiko hayo ni mwendelezo wa mahakama ya Uholanzi ambayo iliagiza Uholanzi katikati ya mwezi wa Februari kusitisha usafirishaji wa sehemu za F-35 kwenda Israel. Ndege mbili za kivita za F-35 zimepigwa picha kwenye kambi ya kikosi cha wanaanga cha Royal Danish Air Force (RDAF) Fighter Wing Skrydstrup, Denmark, Oktoba 1, 2023 (Picha ya kielelezo). AFP - BO AMSTRUP
Matangazo ya kibiashara

"Denmark haipaswi kupeleka silaha kwa Israeli wakati kuna shaka ya kutosha kwamba nchi hii inafanya uhalifu wa kivita huko Gaza," amesema Tim Whyte, katibu mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Action Aid Denmark, mojawapo ya mashirika yaliyowasilisha malalamiko hayo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. . "Tunahitaji maoni ya mahakama kuhusu wajibu wa Denmark," ameongeza.

Malalamiko hayo yaliyotolewa dhidi ya polisi ya taifa na Wizara ya mambo ya Nje, ni mwendelezo wa mahakama ya Uholanzi ambayo iliagiza Uholanzi katikati ya mwezi wa Februari kusitisha usafirishaji wa sehemu za F-35 kwenda Israel. Hatua kama hiyo ilichukuliwa nchini Canada ambapo muungano wa wanasheria na raia wenye asili ya Palestina waliwasilisha malalamiko dhidi ya serikali ya Justin Trudeau.

Nchini Uholanzi, mahakama iliamua kwamba kulikuwa na "hatari ya wazi kwamba ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kibinadamu ya vita utafanywa katika Ukanda wa Gaza" na ndege za kivita za Israeli F-35. Huko Denmark, vyombo vya habari vya uchunguzi Danwatch vilifichua mnamo mwezi Novemba kwamba ndege za Israeli aina ya F-35 zilikuwa na vifaa vilivyotengenezwa na kampuni ya Denmark, Terma.

Vita kati ya Israel na Hamas vilichochewa tarehe 7 Oktoba na shambulio la kiwango kikubwa mno la Hamas ambalo lilisababisha vifo vya takriban watu 1,160 kusini mwa Israel, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo rasmi. Katika kujibu, Israel iliapa kuangamiza Hamas, ambayo inachukuliwa kuwa shirika la kigaidi. Marekani na Umoja wa Ulaya hasa pia wanaichukulia Hamas kuwa shirika la kigaidi. Wizara ya Afya ya Palestina meitangaza Jumanne idadi mpya ya watu 31,184 waliouawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.