Pata taarifa kuu

Vita huko Gaza: Meli ya kwanza inayoleta msaada Palestina yaondoka Cyprus

Meli ya kwanza inayotumia ukanda wa baharini kati ya Cyprus na Ukanda wa Gaza kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo la Palestina inayokabiliwa na njaa iliondoka kwenye bandari ya Cyprus ya Larnaca Jumanne asubuhi, moja ya mashirika mawili yasiyo yakiserikali ynayohusika na operesheni hii limeliambia shirika la habari la AFP.

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Open Arms la Uhispania (picha yetu) "iliondoka" karibu 6:50 asubuhi saa za kimataifa mnamo Machi 12, 2024 kuelekea Gaza.
Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Open Arms la Uhispania (picha yetu) "iliondoka" karibu 6:50 asubuhi saa za kimataifa mnamo Machi 12, 2024 kuelekea Gaza. AP - Petros Karadjias
Matangazo ya kibiashara

Meli ya Shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Open Arms, iliyobeba chakula kitakachosambazwa huko Gaza na shirika la World Central Kitchen, la José Andrés, iliondoka karibu 6:50 asubuhi saa za kimataifa mnamo Machi 12, Laura Lanuza, msemaji wa Open Arms ameliambia shirika la habari la AFP. Meli hii, inayoitwa Open Arms, ina jina sawa na shirika linalotumiwa kuwaokoa wahamiaji katika Bahari ya Mediterania. Ni lazima kubeba kifaa cha jukwaa kinachoelea ili kuwezesha kuteremka kwa misaada ya kibinadamu mara tu itakapofika Gaza kwani hakuna bandari inayofanya kazi katika eneo hilo. Meli hiyo inapaswa kuchukua siku mbili kukamilisha kilomita 370 inayotenganisha Larnaca na Gaza.

Meli hii imebeba takriban tani 200 za chakula (mchele, unga, bidhaa za makopo, n.k.) ambazo zitsambazwa Gaza na shirika la World Central Kitchen (WCK) la mpishi mwenye uraia pacha, Uhispania na Marekani, José Andrés, ambaye tayari amekuwa na timu Gaza tangu kuanza kwa vita, linaandika shirika la habari la AFP.

Mtihani kwa Kupro, tumaini la Gaza

Rais wa Jamhuri, Nikos Christodoulides, amehusika kibinafsi katika uanzishwaji wa ukandaa huu wa kibinadamu, anasema mwandishi wetu maalum huko Cyprus, Sophie Guignon. Ni mtihani kwa Kupro, jimbo dogo la Mashariki ya Mediterania, ambalo lilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004 na ambalo linajipata kuwa kitovu cha tahadhari ya kimataifa katika mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu katika siku za hivi karibuni.

Hata hivyo, chaguo hili la ukanda wa kibinadamu wa baharini hadi Gaza - ingawa linasifiwa - litakuwa na ufanisi mdogo kuliko usafiri wa barabara. Mamia ya malori yanasubiri kuingia Ukanda wa Gaza kupitia Rafah nchini Misri au kupitia kivuko cha Kerem Shalom. Israel, ambayo imekuwa ikilizingira eneo hilo tangu Oktoba 9, 2023, inaruhusu tu misaada kwa kiwango kidogo. Kutokana na hali hiyo, wataalam wengi katika utoaji wa misaada ya kibinadamu wanakubali kwamba ukanda huu wa kibinadamu wa baharini utakuwa mgumu kuzuia baa la njaa huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.