Pata taarifa kuu
KENYA

Mashua inayokisiwa kubeba watu 20 yazama nchini Kenya

Maiti moja imeopolewa huku watu wengine wakihofiwa kufa maji baada ya mashua kuzama katika mto Nzoia huko Budalang'i nchini Kenya.

Eneo linaloripotiwa mashua kuzama na watu kupoteza maisha
Eneo linaloripotiwa mashua kuzama na watu kupoteza maisha Dailynation.com
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Daily nation la Kenya limearifu kuwa Boti hiyo iliondoka katika bandari ya Victoria katika kaunti ya Busia ikielekea katika ufukwe wa mauamau kabla ya ajali kutokea.

Afisa wa serikali katika eneo hilo Alfred Namwakira, amesema boti hiyo ilikuwa na watu 20 ambapo mpaka sasa mwili wa mtoto mmoja umeokolewa wakati jitihada zikiendelea.

Mwanamke mmoja aliyekuwa akisafiri na watoto wake watatu ameokolewa na kuthibitisha kuwa mwili wa mtoto uliokolewa ulikuwa wa mmoja wa watoto wake huku wengine wawili hawajulikani walipo.

Taarifa za awali zinadai kuwa boti hiyo ilikuwa imezidisha uzito uliotakiwa na hivyo bado wanausalama kubaini idadi kamili ya watu waliokuwa katika chombo hicho.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.