Pata taarifa kuu

Mazungumzo kati ya serikali na madaktari kumaliza mgomo wa kitaifa yamekwama

Mazungumzo kati ya serikali ya Kenya na madaktari nchini humo ya kumaliza mgomo ambao umedumu kwa zaidi ya siku 40, yamegonga mwamba, serikali sasa ikitishia kutowalipa madaktari hao mishahara.

Kumekuwepo na mkwamo kati ya madkatari na serikali kuhusu mgomo.
Kumekuwepo na mkwamo kati ya madkatari na serikali kuhusu mgomo. REUTERS - Monicah Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Serikali inatuhumu madaktari kwa kutokuwa waaminifu kushikiniza matakwa yao, huku madaktari wanasisitiza kwamba serikali imekataa kuangazia swala la malipo ya wanafunzi madakatari.

Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za umma wameendelea kukataa mapendekezo ya serikali ya rais William Ruto ilikusitisha mgomo huo ambao umelemaza shughuli katika hospitali hizo raia wakiendelea kuhangaika.

Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara.
Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara. REUTERS - Monicah Mwangi

Karibia wanachama elfu saba kutoka chama cha madaktari (KMPDU) walianza mgomo wa kitaifa katikati ya mwezi Machi mwaka huu kuishinikiza serikali kuwapa malipo bora pamoja na kudumisha mazingira yao ya kazi.

Davji Atellahni ni katibu mkuu wa muungano wa madaktari nchini kenya.

“Hatutakubali ukiukaji wa sheria na njama yoyote ya serikali , tunafahamu kwamba pesa tunazodai serikali kwa ajili ya madakatari wanafunzi ni kiasi cha burudani ya marupurupu ya hao mawaziri.” alisema Davji Atellahni ni katibu mkuu wa muungano wa madaktari nchini kenya.

00:33

Davji Atellahni ni katibu mkuu wa muungano wa madaktari nchini kenya

Malipo duni na mazingira ya kufanya kazi nchini Kenya, imepelekea baadhi ya wadhumu wa afya kuondoka kwenye taifa hilo kwenda kutafuta ajira katika mataifa mengine ya Afrika yakiwemo yake ya bara Ulaya.

Mwaka wa 2017, madaktari walishiriki mgomo wa kitaifa wa siku 100, hatua ambayo ilisababisha kufungwa kwa hospitali kwa umma wagonjwa wengi wakitaabika kupata huduma za matibabu.

Soma piaKenya: Madaktari wanaogoma wakataa pendekezo la serikali la nyongeza ya mshahara

Wagonjwa kadhaa waliripotiwa kufariki wakati wa mgomo huo wa siku 100 ambao ulimalizika baada ya makubaliano kuafikiwa kati ya serikali na vyama vya madaktari.

Madaktari wanaituhumu serikali kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya sehemu za makubaliano hayo hali ambayo imechangia kutokea kwa mgomo wa sasa.

Serikali imetishia kuwachukulia hatua madaktari wanaoendelea kugoma licha ya agizo la mahakama la kuwataka kurejea kazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.