Pata taarifa kuu
MVUA-UHARIBIFU

Nchi za Afrika Mashariki zaendelea kukumbwa na mafuruko, Themanini wafariki Kenya

Watu karibu 80 wamepoteza maisha baada ya kusombwa na maji ya mafuriko nchini Kenya, kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha hasa katika jiji kuu Nairobi.

Hali ya mafuriko katika mitaa ya jiji la Nairobi nchini Kenya.
Hali ya mafuriko katika mitaa ya jiji la Nairobi nchini Kenya. twitter.com/hashtag
Matangazo ya kibiashara

Naibu rais Rigathi Gachagua, amewatembelea baadhi ya watu walioathiriwa na mafuriko jijini Nairobi, na kuwataka raia wa nchi hiyo kuachana na tabia zinazohatarisha maisha yao, kipindi hiki cha mvua.

Mbali na Kenya, Tanzania pia imeshuhudia changamoto hii ya mafuriko, ambapo serikali imesema, watu zaidi ya 150 wamepoteza maisha, huku mitaa kadhaa ikijaa maji hasa jijini Dar es salaam.

Mji wa Kalemie nchini DRC na baadhi ya maeneo nchini Burundi pia yanaendelea kushudia mafuriko makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.