Pata taarifa kuu

Mvua zaendelea kunyesha Afrika Mashariki, Serikali ya Kenya yaahirisha ufunguzi wa shule hadi Mei 6

Nchi za Afrika Mashariki, zinatarajiwa kuendelea kushuhudia mvua kubwa  kwa mujibu wa mamlaka za utabiri wa hali ya hewa, wakati huu mvua inayonyesha ikiendelea kusababisa maafa na uharibifu mkubwa.

Moja ya familia jijini Nairobi yalazimika kutoroka makazi yao kufuati mafuriko ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Githurai jijini Nairobi, Kenya, Jumatano, Aprili 24, 2024.
Moja ya familia jijini Nairobi yalazimika kutoroka makazi yao kufuati mafuriko ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Githurai jijini Nairobi, Kenya, Jumatano, Aprili 24, 2024. AP - Patrick Ngugi
Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya serikali imetangaza kuahirishwa kufunguliwa kwa muhula wa pili wa Shule hadi tarehe SITA mwezi Mei kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha ambayo imesababisha vifo vya watu karibu 80.

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amesema katika taarifa kuwa baadhi ya shule zimeathirika pakubwa na mafuriko,hali ambayo amesema huenda ikahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu katika shule hizo.

“Ripoti ambazo wizara ya elimu imepokea kutoka kwa asasi mbali mbali za serikali, zinabainisha kwamba shule nyingi katika maeneo tofauti nchini Kenya, zimeathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. Kwa sababu hii Wizara ya Elimu imeahirisha ufunguzi wa shule za msingi na upili kwa wiki moja hadi Jumatatu 6, Mei, 2024,” imesema wizara ya elimu.

Waziri alisema wizara yake itashirikiana na wadau wote katika kuchukua hatua za kukabili athari za mvua kubwa inayonyesha kwa sasa.

Hayo yanajiri huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikionya kuwa mvua kubwa itaendelea kushuhudiwa nchini katika siku chache zijazo, huku zaidi ya watu 90 wakiripotiwa kufariki na wengine kujeruhiwa au kutoweka.

Nchini Tanzania, serikali imeendelea kutoa tahadhari baada ya watu zaidi 150 kupoteza maisha kutokana na mafuriko kutokana na mvua inayosababishwa na mfumo wa Hali ya Hewa iitwayo El Nino ambayo pia inanyesha nchini DRC na Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.