Pata taarifa kuu
BURUNDI-RPA-SIASA-SHERIA

Mkurugenzi wa redio RPA ahamishiwa katika jela la Muramvya

Mkurugenzi wa redio RPA inayosikilizwa na watu wengi nchini Burundi, Bob Rugurika ameondolea katika jela kuu la Mpimba na kupelekwa moja kwa moja katika jela la Muramvya katikati mwa Burundi.

Picha ya Christian Butoyi, mwenye umri wa mika 33, anaedaiwa kuwaua watawa watatu kutoka Italia, wakati akionyeshwa na polisi mbele ya vyombo vya habari mjiniBujumbura, Septemba 9 mwaka 2014.
Picha ya Christian Butoyi, mwenye umri wa mika 33, anaedaiwa kuwaua watawa watatu kutoka Italia, wakati akionyeshwa na polisi mbele ya vyombo vya habari mjiniBujumbura, Septemba 9 mwaka 2014. RFI/Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Uamzi wa kuhumishwa kwa mkurugenzi huyo wa RPA ulichukuliwa na Afisa wa Ofisi ya mashitaka mjini Bujumbura, Emmanuel Nkurikiye, bila hata hivyo wanasheria wake aidha familia yake kufahamishwa.

Wengi wanahisi kwamba Bob Rugurika angelipelekwa eneo kusikojulikana. Gari iliyombeba hadi mkoani Muramvya ni ya  Wizara ya sheria ambayo imekua imeondolewa namba ya usajili.

Bob Rugurika alikamatwa na kupelekwa katika jela kuu la Mpimba Jumanne 20 jioni, baada ya kuitika hati iliyotolewa na afisa katika ofisi ya mwendesha mashitaka katika manispaa ya jiji la Bujumbura, Emmanuel Nkurikiye, ambaye alimtaka amfikishe mikononi mwa vyombo vya sheria, mtu mmoja aliyekiri kuhusika na mauaji ya watawa watatu kutoka Italia waliouwawa tarehe 7 na 8 Septemba mwaka 2014, katika wilaya ya Kamenge mjini Bujumbura.

Redio RPA iliendesha uchunguzi kuhusu mauaji hayo, na tangu wiki iliyopita redio hio imekua ikiweka wazi matokeo ya uchunguzi wake, ambapo mtu huyo aliyekiri kuhusika katika mauaji hayo, aliwanyooshea kidole baadhi ya maafisa wakuu katika Idara ya Ujasusi ya Burundi pamoja na polisi, akibaini kwamba wao ndio waliomuagiza akishirikiana na watu wengine (ambao aliwataja majina) kutekeleza mauaji ya watawa hao.

Mtu huyo aliyehojiwa na redio RPA, alimtaja mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Ujasusi ya Burundi, Adolphe Nshimirimana, akibaini kwamba ni mmoja kati ya maafisa wa Idara ya Ujasusi na polisi walioandaa mpango huo wa kuwamalizia maisha watawa hao kutoka Italia.

Hata hivyo katika uchunguzi wake, RPA, ilibaini kwamba ilijaribu kuwatafuta watu wote waliotajwa katika kesi hiyo, baadhi walikanausha tuhuma dhidi yao, na wengine walisema kwamba wanasubiri uchunguzi wa vyombo vya sheria vya Burundi.

Bob Rugurika alihojiwa kwa muda wa saa 8 kabla ya kupelekwa katika jela kuu la Mpimba. Bob Rugurika amesema kama chombo cha habari, na kulingana na sheria za uandishi wa habari, RPA, iliendesha uchunguzi wake bila hata hivyo kuingilia vyombo vya sheria katika uchunguzi wake, ili kujaribu kutoa mwanga kuhusu mauaji hayo.
Mamia kwa maelfu ya watu walikua wamejielekeza katika Ofisi ya mashitaka mjini Bujumbura ili kusikiliza atakacho hojiwa mkurugenzi huyo wa RPA.

Afisa katika Ofisi ya mashitaka anamtuhumu Bob Rugurika kwamba hakutoa ushiriki wake kwa vyombo vya sheria, kuingilia kazi za vyombo vya sheria wakati kesi ilikua katika hatua ya uchunguzi, na kushiriki katika mauaji ya watawa hao watatu kutoka Italia.

Mkurugenzi wa redio RPA anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela, iwapo atapatikana na hatia.
Polisi ya Burundi ilimkamata mtu mwenye ugonjwa wa akili, ikimtuhumu kuhusika katika mauaji ya watawa watatu waliouawa tarehe 7 na 8 septemba mwaka 2014 wilayani Kamenge mjini Bujumbura.

Redio RPA imeendelea kurusha matokeo ya uchunguzi wake, licha ya kuwa mkurugenzi wake anazuiliwa jela.

Vyama vya waandishi wa habari vimebaini kwamba vina imani kuwa Bob Rugurika ataachiliwa huru, kwani hana hatia. Vyama hivyo vimetisha kuchukua umazi mkali iwapo utawala utaendelea kumzuia jela mkurugenzi huyo wa redio RPA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.