Pata taarifa kuu
CAMEROON-BOKO HARAM-SHAMBULIO-USALAMA

Cameroon: mashambulizi ya kujitoa mhanga yatokea Maroua

Mashambulizi ya kujitoa mhanga yametokea katika mji wa Maroua, mji mkubwa wa kaskazini mwa Cameroon. Watu wawili wa kujitoa mhanga wamelipua vilipuzi katika maeneo mawili tofauti ya mji huo, ikiwa ni pamoja na soko.

Miili ya watu waliouawa yaondolewa katika soko la Maroua, Julai 22 mwaka 2015.
Miili ya watu waliouawa yaondolewa katika soko la Maroua, Julai 22 mwaka 2015. Journal du Cameroun / David Wanedam
Matangazo ya kibiashara

Watu wengi wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa. Milipuko hiyo ilitokea saa 9:30 saa za Cameroon (sawa na saa 7:30 saa za kimataifa). Maroua ambayo ni makao makuu ya operesheni dhidi ya Boko Haram ni eneo muhimu la jeshi la Cameroon, Kaskazini mwa nchi ya cameroon.

Milipuko hiyo miwili iliotokea kwa wakati mmoja kwenye umbali wa mita 800 umezua hali ya wasiwasio katika mji wa Maroua mapema Jumatano mchana wiki hii. Mlipuko wa kwanza ulilenga katika soko kuu la mji hu, mahali kunakotembelewa na watu wengi. mlipuko wa pili umetokea katika wilaya ya Barmaré.

Magaidi ni wasichana wawili walio na umri wa chini ya miaka kumi na tano, ambao walikuwa wakiomba katika soko, amesema mkuu wa jimbo hilo.

Wasichana hao waliku wakivalia mijitandio, licha ya marufuku iliyotolewa wiki iliyopita ya kuvaa hijabu au mijitandio katika sehemu hiyo ya nchi, kutokana na hatari ya mashambulizi. Ripoti iliyotolewa katika taarifa ya Ikulu ya raisimesema watu 13 wameuawa, ikiwa ni pamoja na wasichana hao waliojitoa mhangai, na wengine 32 wamejeruhiwa.

Baada ya mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika mji wa Fotokol juma lililopita, hii ni mara ya pili Cameroon kukabiliwa na mashambulizi kama haya.

Hakuna kundi hata moja ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo, lakini kundi la Boko Haram linashukiwa kuendesha shambulio hilo.

Hata hivyo Boko Haram imekua imekua ikiendesha mashambulizi ya hapa na pale katika nchi za Cameroon, Nigeria, Niger na Chad. Boko Haram ni tishio kwa usalama wa Ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.