Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 50,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano kaskazini mwa Ethiopia

Zaidi ya watu 50,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano katika eneo linalozozaniwa la kaskazini mwa Ethiopia, Umoja wa Mataifa umesema, siku kumi baada ya kuanza kwa mapigano kati ya wapiganaji kutoka mikoa ya Tigray na Amhara.

Wanawake waliokimbia makazi yao wakisubiri wakati wa usambazaji wa chakula ulioandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika kijiji cha Adlale, karibu na mji wa Gode, Ethiopia, Aprili 6, 2022.
Wanawake waliokimbia makazi yao wakisubiri wakati wa usambazaji wa chakula ulioandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika kijiji cha Adlale, karibu na mji wa Gode, Ethiopia, Aprili 6, 2022. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizi mpya zinasababisha wasiwasi wa kimataifa. Siku ya Jumamosi, balozi kadhaa nchini Ethiopia, zikiwemo Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Marekani, zilisema "zinasikitishwa na ripoti za ghasia katika maeneo yanayozozaniwa kaskazini mwa Ethiopia", na "zimetoa wito wa kusitishwa kwa ghasia na ulinzi wa raia."

"Idadi ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano katika mji wa Alamata na woredas (kitengo kidogo cha utawala) cha Raya Alamata, Zata na Ofla tangu Aprili 13 na 14 imefikia zaidi ya watu 50,000," shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema katika ripoti iliyochapishwa Jumatatu jioni, liikinukuu mamlaka za ndani.

Takriban 42,000 kati yao walikimbia kuelekea kusini, haswa karibu na mji wa Kobo, na 8,300 kuelekea eneo la Sekota kaskazini, imebaini OCHA, ikibainisha kwamba wengi wa watu waliohamishwa ni "wanawake, watoto, vijana na wazee.

Alamata na wilaya jirani ziko katika ukanda wa Raya, unaozozaniwa kati ya mikoa ya Tigray na Amhara, ambapo mapigano kati ya wapiganaji wa makabila haya mawili yalizuka takriban siku kumi zilizopita. Yakiwa yameunganishwa kiutawala na Tigray katika miaka ya 1990, maeneo ya Raya (Tigray kusini) na yale ya Wolkait (Tigray magharibi) yamedaiwa kwa miongo kadhaa na kabila la Amhara.

Wanamgambo na "vikosi maalum" kutoka mkoa wa Amhara waliingia katika maeneo hayo mnamo Novemba 2020, wakati mzozo ulipozuka kati ya mamlaka ya Tigray ya Tigray People's Liberation Front (TPLF) na serikali ya shirikisho, na kuweka utawala wao wenyewe. Kulingana na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya serikali ya shirikisho na TPLF mnamo mwezi Novemba 2022 huko Pretoria, vikosi vya Amhara vilipaswa kuondoka.

"Kukuza" mahitaji ya kibinadamu

Utambulisho kamili wa wapiganaji waliohusika katika mapigano ya hivi majuzi bado haujulikani. Siku ya Jumatano Aprili 17, mamlaka ya eneo la Amhara ilishutumu TPLF kwa "kufanya uvamizi (...) kinyume kabisa na makubaliano ya Pretoria", na kutaka vikosi hivi "viondoke haraka katika maeneo wanayodhibiti" .

Siku moja kabla, rais wa utawala wa muda wa Tigray, Getachew Reda, alizungumza kwenye X kuhusu "matukio ya kusini mwa Tigray, na maeneo mengine yanayokaliwa". Alithibitisha kwamba hayakutokana na "mgogoro kati ya serikali ya shirikisho na utawala wa mpito/au TPLF", wala "mgogoro kati ya tawala za Tigray na Amhara" bali ni uhasama wa "maadui wanaopinga makubaliano ya Pretoria".

Ingawa misaada ya awali ya kibinadamu imetumwa na serikali ya shirikisho na mashirika yasiyo ya kiserikali, "majibu hayakidhi mahitaji yanayoongezeka," inaongeza OCHA.

Hali ya dharura

Wafuasi wa taifa la Amhara wamekuwa katika mzozo na serikali kuu tangu kutangazwa mwezi Aprili 2023 na mamlaka ya Addis ya kutaka kusambaratisha "vikosi maalum", vikosi haramu vya kijeshi vilivyoanzishwa na mataifa kadhaa ya kikanda nchini Ethiopia kwa takriban miaka kumi na tano. Wazalendo wa Amhara wanaishutumu serikali kwa kutaka kudhoofisha eneo lao.

Tangu wakati huo, mapigano yameripotiwa mara kwa mara kati ya wanamgambo na "vikosi maalum" vya Amhara - ambao walikuwa mshirika mkuu wa jeshi la Ethiopia dhidi ya waasi wa Tigray  waliokuwa wakipigana dhidi ya jeshi. Kutokana na ongezeko la ghasia, serikali ya shirikisho ilitangaza hali ya hatari mnamo Agosti 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.