Pata taarifa kuu
CAMEROON-NIGERIA-CHAD-BOKO HARAM-Usalama

Cameroon: hali ya wasiwasi yatanda Fotokol

Ni wiki moja sasa, siku baada ya siku, tangu kundi la Boko Haram lianzishe mfululizo wa mashambulizi katika mji wa Fotokol, kaskazini mwa Cameroon.

Kijiji kinacho pakana  na Fotokol, ambacho kiliharibiwa wiki iliyopita na mashambulizi ya Bokom Haram.
Kijiji kinacho pakana na Fotokol, ambacho kiliharibiwa wiki iliyopita na mashambulizi ya Bokom Haram. RFI/OR
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalitokana na operesheni iliyofanywa na majeshi ya Cameroon na Chad dhidi ya Boko Haram. Washambuliaji walikuja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri, na kuua raia wa kawaida 81, ikiwa ni pamoja na waumini 30 kutoka dini ya Uislamu katika Msikiti, kabla ya kutimuliwa na jeshi. Wiki moja baada ya tukio hilo wakazi wa kijiji hicho wamebaki katika hali ya wasiwasi na simanzi.

Kijiji hicho cha Fotokol chenye wakazi takribani 3000 kinakabiliwa na hali ya sintofahamu, baada ya mashambulizi ya Boko Haram, ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 80, usiku wa Jumatano kumankia Alhamisi Juma lililopita.

Mashambulizi hayo yalitikea wakati ambapo wanajeshi wa Chad walikua waliondoka kwenye ngome zao walizokua wakishikilia upande wa pili wa mpaka, nchini Nigeria katika mji wa Gambaru.

Mkuu wa bataliani ya wanajeshi wa Cameroon, Beltus Kouéné, ameelezea masikitiko yake kuona kulikosekana uratibu na mawasiliano kati ya majeshi yao na yale ya Chad.

" Ninachoweza kukuambia kuhusiana na mashambulizi ya Februari 4 mwaka 2014 ni kwamba adui bila shaka alipata fursa ya kupenya na kuanzisha mashambulizi hayo baada ya wanajeshi wetu na wale wa Chad kutokuelewana kuhusu utaratibu ambao wanaweza kutumia kwa kukabiliana na masghambulizi ya Boko Haramu", amesema Beltus Kouéné.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.