Pata taarifa kuu
DRCONGO-MAUAJI

Serikali ya Kivu Kusini kupiga kambi eneo la mauaji

Gavana wa jimbo la Kivu ya kaskazini Julien Paluku amebaini maskitiko yake kuhusu matukio ya mauaji yanayoendelea kuripitiwa katika baadhi ya maeneo hususan kusini mwa mtaa wa Lubero ambako watu walikuwa wakieshi pamoja kwa kushirikiana. Kiongozi huyo amesema wamepigwa na butwaa kuhusu kuibuka kwa mauaji ya Kikabila hivi karibuni.

Julien Paluku Kahongwa, gavana wa Mkoa wa Kivu ya Kkaskazini mashariki mwa DRCongo.
Julien Paluku Kahongwa, gavana wa Mkoa wa Kivu ya Kkaskazini mashariki mwa DRCongo.
Matangazo ya kibiashara

Hatuwa kadhaa za usalama zimechukuliwa na viongozi wa mkoa wa Kivu ya Kusini kuhakikisha Usalama unaimarika na wahusika wa mauaji wanatiwa nguvuni na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Akizungumza na idhaa ya kiswahili ya Radio France Internationale, Gavana Paluku amesema kwa sasa kamati ya Usalama ya jimbo la Kivu ya Kusini, wabunge na wadau mbalimbali wanaelekea Miriki kuhakikisha wanafaham chanzo cha mauaji yanayoendelea ili wapatishie suluhu ya kudumu.

Paluku amesema badala ya kubaki mjini Goma wameona ni vema kupiga kambi katika eneo la tukio ili kufahamu zaidi hali ya mambo, hususan matatizo yanayo sababisha hali ya usalama kuvunjika mara kwa mara.

Watu wanaokadiriwa kufikia kumi na tano wameuawa kutokana na mapigano kati ya makundi ya wapiganaji mashariki mwa kongo, mapigano yanayotajwa kuwa ni yakikabila.

Mamlaka kwenye eneo hilo zinasema kuwa mapigano hayo yametokea kwenye kijiji cha Mukeberwa, jimboni Kivu Kaskazini, ambapo Umoja wa Mataifa unasema kuwa mapigano hayo yametokana na mzozo wa kikabila unaoendelea kufukuta kwenye eneo hilo.

Umoja wa Mataifa umebaini kuwa mapigano haya ni kati ya watu wa makabila la wahutu na Wanande na kuungwa mkono na baadhi ya makundi hali ambayo inafanya mapigano hayo kuwa mabaya zaidi.

Wahutu wanaungwa mkono na kundi la waasi wa Rwanda FDLR, huku wale wa Nandi wakiungwa mkono na wapiganaji wa Mai-Mai

Ofisi ya tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa imetoa wito kwa Serikali ya DRC kuhakikisha inatoa ulinzi kwa raia wake na kumaliza vitisho vya makundi haya ya wapiganaji.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.