Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-UKIMWI-Afya

Australia : mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imetolewa kuelekea mkutano wa 20 duniani wa ukimwi utakaoanza Jumapili mjini Melbourne nchini Australia na kubaini kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na ukimwi duniani vimepungua kwa kasi mwaka 2013 sawa na asilimia 11.8% ndani ya mwaka mmoja.

Maambukizi ya ukimwi yamepongua duniani.
Maambukizi ya ukimwi yamepongua duniani. Travel Ink
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, ripoti hiyo inamaanisha kwamba lengo la pambano hilo mwaka huu ni kusisitiza kuwahudumia ambao wamesahauliwa kama vile wafungwa, wafanyabiashara ya ngono, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kadhalika.

Hii ni idadi ya waathiriwa wa ukimwi duniani ambayo imetolewa na taasisi ya Umoja wa Mataifa inayokabiliana na ukimwi katika ripoti ya mwaka 2013, kabla ya kikao cha Melbourne kuhusu ukimwi.

Kwa jumla mwaka 2013, takribani watu milioni 35 walikua wakiishi na virus vya ukimwi duniani, huku watu milioni 1.5 walifariki kutokana na ukimwi mwaka 2013.

Mwaka huo huo wa 2013, watu milioni 2.1 duniani waliambukizwa virus vya ukimwi, huku idadi hio ikishuka mwaka 2001 kwa asilimia 38.

Watoto 240.000 walizaliwa na virus vya ukimwi mwaka 2013, huku asilimia 87.7 wakiwa ni watoto kutoka katika nchi za Afrika ziliyoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Eneo hili lilioko kusini mwa jangwa la Sahara linaendela kuathirika zaidi na ugonjwa huu wa ukimwi, likiwa na asilimia 70.6 ya watu walioathirika duniani. Ugonjwa huu unawaathiri kwa sehemu kubwa wanawake ambao wamefikiya sasa asilimia 58 ya walioambukizwa katika eneo hili la kusini mwa jangwa la sahara.

Ugonjwa wa kifua kikuu ni moja ya sababu kuu ya vifo kwa watu wanaoathika na virus vya ukimwi.

Dola bilioni 19.1 ziliwekezwa mwaka 2013 kwa kupambana na ugonjwa wa ukimwi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.